Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » DOGO JANJA AMPIGIA MAGOTI MADEE ILI AMRUDISHE TENA TIP TOP CONNECTION

DOGO JANJA AMPIGIA MAGOTI MADEE ILI AMRUDISHE TENA TIP TOP CONNECTION

tangazo

Kuna kila ishara kuwa meli ya Watanashati Entertainment iliyomchukua Dogo Janja kwa mbwembwe nyingi, inaelekea kuzama na abiria wawili waliosalia, Dogo Janjaro na PNC wameanza kutafuta maboya haraka kujihami.


Kwa mujibu wa meneja wa Tip Top Connection, Babu Tale, Dogo Janja amekuwa akimpigia simu Madee ili wakae chini waongee kumaliza tofauti zao na ili arejee Tip Top.

“Unavyomwona Dogo Janja leo hii anampigia simu Madee kumwomba wakae chini,” alisema Tale kwenye kipindi cha Mkasi.
 
“Ni kwamba wale marafiki hawapo tena. Leo hii kwakuwa Dogo Janja anamhitaji Madee atausema ukweli. Dogo Janja hela yake alikuwa anampa mshkaji mmoja anaitwa Doka. Mimi niliyajua hayo baada ya matatizo.”

Dogo Janja alijiondoa Tip Top June mwaka jana kwa madai kibao ikiwa pamoja na kudai kwamba hakuwahi kusaidiwa chochote na Madee zaidi ya mambo ya muziki pekee huku kula, malazi na ada ya shule vikifanywa na rafiki yake Madee aitwaye Abdallah Doka ambaye (Dogo Janja) alikuwa akiishi kwake.
 
Alidai kutokana na ngoma zake kujipatia umaarufu alikuwa akipata show nyingi nchini na zote alikuwa halipwi chini ya milioni moja. Kilichokuwa kinamsikitisha anasema ni kulipwa hela kidogo isiyozidi laki mbili na hivyo kumfanya aishi kwa tabu licha ya kuingiza hela nyingi za show.
 
“Nilikuwa navumilia tu, kwasababu kila nilipolalamika kuhusu mambo ya hela Madee alikuwa mkali sana,” alikaririwa kwenye kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger