Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » MWANAUME ALIYEKIRI KUCHANGIA MKE NCHINI KENYA ATIMULIWA KAZI....

MWANAUME ALIYEKIRI KUCHANGIA MKE NCHINI KENYA ATIMULIWA KAZI....

tangazo
 
Mwanaume wa nchini Kenya ambaye aliridhia kusaini mkataba wa kuchangia mwanamke mmoja na mwanaume mwenzake amefukuzwa kazi na bosi wake.


Mwanaume huyo Sylvester Mwendwa, ambaye mwishoni mwa wiki alitangaza hadharani penzi lake hilo la mkataba na mwanamke mjane, amesema bosi wake amemfukuza kazi ya bucha aliyokuwa akiifanya baada ya kusikia habari hiyo.

Mwendwa ambaye alikiri kuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanamke huyo na yuko radhi kufanya lolote ili aendelee kuwanae hata ikibidi kuchangia na mwanaume mwingine, amedai amekuwa akipokea ujumbe wa kutishiwa maisha yake.

Baada ya uhusiano wake na mwanamke huyo Joyce Wambui pamoja na mwanaume mwingine kujulikana kwa umma Mwendwa sasa amelazimika kukimbilia mafichoni akihofia usalama wa maisha yake.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger