tangazo
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amesema hata kama
msanii Nay wa Mitego akiwa na mpenzi mwigine kwa sasa lakini anajivunia
kupendwa na kijana huyo kwani alihangaika sana kumpata.
Akizungumza
na mwandishi wetu, Nisha alisema Nay alimfuatilia kwa kipindi kirefu na
alimzungusha kama miaka miwili kabla hata hajawa staa.
“Nikivuta ile
picha ya kumdengulia kiasi kile mpaka kuamua kumkubali, naamini
alinipenda tu na hata kama hakunipenda lakini najivunia kwamba
alihangaika kunipata,” alisema Nisha.
Wawili hao walidumu katika uhusiano wa kimapenzi kwa miezi kadhaa kabla ya kuachana na kila mmoja akichukua hamsini zake.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.