Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » AISHA BUI AKANUSHA MADAI YALIYOSAMBAA KWAMBA " YEYE NI PUNDA " ALIYEFUNGWA BRAZIL

AISHA BUI AKANUSHA MADAI YALIYOSAMBAA KWAMBA " YEYE NI PUNDA " ALIYEFUNGWA BRAZIL

tangazo

Msanii  wa Bongo Movie Aisha Bui amefunguka kuwa ameshangazwa na madai yaliyoenea kuwa amefungwa nchini Brazil baada ya kunaswa na unga. 

Akizungumza na Globalpublishers, Aisha amesema kuwa yeye alimfuata mchumba  wake nchini Brazil na alipoondoka nchini Tanzania aliondoka kimya kimya maana alijua ni lazima watu watazusha mambo na kumpaka matope ya kumchafua. 

"Jamani hayo madai ya kwamba mimi nimefungwa huku(Brazil) kwa kesi ya madawa ya kulevya hata mimi mwenyewe nayashangaa, nipo huku kwa mwezi wa nne sasa nimekuja kwa mchumba wangu. hizo taarifa za kwamba eti nimefungwa ni uzushi unaotengenezwa kwa nia ya kunichafua tu".Alisema Aisha  na  kuongeza

"Wakati naondoka Tanzania ilikuwa kimya kimya kwakuwa nilijua kuna baadhi ya watu watazusha mambo ya kunipaka matope na ndicho walichofanya. Naomba watanzania wajue niko huru kabisa naendelea na shughuli zangu kama kawaida, natarajia kurudi Bongo hivi karibuni"

TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger