Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » Chege na Temba kuanza ziara ya miezi 3 Ulaya wiki ijayo.Ommy Dimpoz naye yuko Marekani.

Chege na Temba kuanza ziara ya miezi 3 Ulaya wiki ijayo.Ommy Dimpoz naye yuko Marekani.

tangazo
 
Wasanii wa Kundi la TMK Wanaume Family Chege na Temba wanatarajia kuanza ziara ya miezi 3 barani Ulaya kuanzia wiki ijayo.

Akizungumza na mwandishi wetu, meneja wa kundi hilo Said Fella amesema leo ndio wanategemea kupata Visa na wiki ijayo (September 25) Chege na Temba wataondoka nchini wakielekea nchini Sweeden ambako watafanya show ya kwanza (October 5). 

Temba na Chege watashiriki show za Serengeti Fiesta Musoma siku ya Ijumaa hii na kumalizia Shinyanga siku ya Jumapili zikiwa ndio show zao za mwisho za Fiesta kabla ya kuondoka nchini .

Msanii mwingine wa Bongo Ommy Dimpoz aliondoka nchini Jana kuelekea Marekani ambako atakuwa na show kadhaa kabla hajarejea nchini kushiriki fainali ya Serengeti Fiesta Dar es salaam, huku Diamond Platnumz naye anatajaria kwenda nchini Malaysia wiki ijayo ambako atafanya show (September 20)
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger