Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » Kundi la AL SHABAAB ladai kuhusika na mauaji ya watu 30 nchini Kenya leo

Kundi la AL SHABAAB ladai kuhusika na mauaji ya watu 30 nchini Kenya leo

tangazo

Kundi la wanamgambo wa kiisilamu la Al shabaab nchini Somalia limedai kutekeleza mauaji ya watu zaidi ya thelathini nchini Kenya kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari nchini Kenya ( Citizen TV) na pia kupitia kwa ukurasa wake wa Twitter.
 
Shirika la habari la Reuters pia limesema kuwa Al Shabaab linasema kwamba Kenya ilipuuza mara kwa mara vitisho vya kundi hilo kuishambulia.

Taarifa kutoka Ikulu ya Rais Kenya zinasema kuwa mshukiwa mmoja amekamatwa. Mshukiwa huyo amejeruhiwa na anapokea matibabu hospitalini.
 
Wanamgambo wa Al Shabaab wanasema kuwa Kenya haikuchukulia kwa uzito onyo walilotoa kwa taifa hilo kwa hatua ya kuwapeleka wanajeshi wake nchini humo kupambana dhidi yao.

Kundi hilo limesema limekuwa likitoa onyo mara kwa mara kwa Kenya kuwa ikiwa haitaondoa vikosi vyake nchini Somalia, athari zitakuwa mbaya mno.
 
Kupitia mtandao wao wa Twitter, Al Shabaab limesema kuwa Kenya ilijidai kutosikia onyo hizo, na kuendelea kuwaua waisilamu wasio na hatia nchini Somalia.
 
Taarifa hiyo ya Twitter ilisema kuwa Shambulio la Westgate ni tone katika bahari tu ya mfano wa yanayowakumba wasomali waisilamu nchini Somalia.
 
Taharuki ilianza hii leo saa saba mchana wakati watu wanaokisiwa kuwa kumi walipovamia jengo la kifahari la Westgate la kuwapiga risasi kiholela wakenya waliokuwa wanaendelea na shughuli zao za kawaida.

Kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu , takriban watu 30 walifariki kwa kupigwa risasi au kutokana na majeraha yao na wengine wengi wenye majeraha ya risasi kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.

-BBC
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger