Mwandishi wa gazeti la MWANANCHI akatwa katwa mapanga mkoani SINGIDA
tangazo
Mwandishi
wa habari wa gazeti la The Citizen na mwananchi mkoani Singida, Awila
Silla amenusurika kuuawa na mtu anayedhaniwa kuwa Jambazi baada ya kukatwa
katwa mapanga kichwani na kusababisha kuzirai. Tukio hilo limetokea juzi saa
mbili usiku jirani na mahakama ya mwanzo ya Utemini mjini Singida.
Awila
ambaye amelazwa wodi 2 katika hospitali ya mkoa amedai kuwa baada ya kukutana na
kijana huyo aliamuriwa kutoa fedha na baada ya kudai hana, jibu hilo
lilisababisha kijana huyo kuanza kumkata Mapanga na alipoangauka na
kuzirai alinyang’anywa simu yake ya kiganjani .
Hata hivyo Awila amedai
kuwa bado hajatoa taarifa ya tukio hilo polisi
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK