tangazo
Mwanamziki mkongwe wa Hip hop na Bongo Fleva,
ambaye pia ni mfalme wa Rymes, Selemani Msindi (Afande Sele), jana amejiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
baada ya kukabidhiwa kadi ya chama hicho na Powell Mfinanga wakati wa
mkutano mkubwa uliofanyika katika kata ya Mafiga na Misufini mkoani
Morogoro...
Muda mfupi kabla ya mkutano huo kuanza, Afande Sele alitupia ujumbe wa kuthibitisha kujiunga na CHADEMA katika ukurasa wake wa facebook uliosomeka:
Quote: Hakuna kusanda,hakuna kumbwanda,mbele kwa mbele makamanda,vua gamba vaa gwanda kisha kaza mkanda, wanashuka sisi tunapandaaa,,,,
Leo tunaanza kuandika historia mpya ktk mkoa wetu wa morogoro na tz kwa ujumla kwa sababu nikiwa kama msanii wa muda mrefu na mfalme pekee wa mzk wa kizazi kipya ninaetunga nyimbo zangu kwa kuzingatia ujumbe muhimu ktk jamii kwa mambo ya kisiasa,kiuchumi,elimu,amani na upendo nk..
Sasa leo nimeamua kwa ridhaa yangu iliyosukumwa na uzalendo na mapenz makubwa kwa taifa langu kuchukua kadi ya kujiunga rasmi uanachama wa CHADEMA..
Tukio hilo kubwa litafanyika leo jioni ktk mkutano wa hadhara utakaofanyika kata yetu ya mafiga/misufini na utahudhuriwa na viongoz mbalimbali wa chama kutoka makao makuu ya chama Dsm pamoja na mbunge wa nyamagana mh Ezekiel Wenje..
Kwa wakaz wa Moro wazalendo nyote mnakaribishwa saaana, ahsanteni wana’ndugu, siasa si uadui, tupingane/tusipigane, Pendo moja!,,,,


