Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » Hali ya mwanamke aliyetandikwa risasi na polisi jijini Arusha yazidi kuwa tete.

Hali ya mwanamke aliyetandikwa risasi na polisi jijini Arusha yazidi kuwa tete.

tangazo
 
HALI ya mwanamke aliyepigwa risasi na polisi katika Benki ya CRDB mjini hapa, Violet Lyapa (30) bado ni tete huku taarifa zake zikifanywa kuwa siri kubwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hospitali ya Selian, Violet bado amelazwa katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU) huku hali yake ikibadilikabadilika.

Pamoja na kwamba tukio hilo limechukua siku zaidi ya tano bado hali ya Violet inafanywa kuwa siri nzito.
 
Mwanamke huyo amewekewa ulinzi mkali katika wodi aliyolazwa lakini mmoja wa wauguzi wa hospitali hiyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe, amesema hali ya majeruhi huyo imekuwa ikibadilika kiasi cha kulazimika kumpa uangalizi maalum.


Jeshi la polisi mkoani Arusha  limekuwa na kigugumizi kutoa taarifa juu ya tukio hilo na hatua zipi zimechukuliwa juu ya uhalali wa umiliki wa silaha iliyotumia kuwatishia polisi baada ya kukuta gari lake limetolewa upepo.
 
Aidha, katika hali inayotia shaka kigogo wa ngazi za juu mkoani Arusha amekuwa akimjulia hali mara kwa mara majeruhi huyo hasa nyakati za usiku na taarifa zilizoenea zinasema kigogo huyo ana uhusiano wa karibu na majeruhi huyo.

Pia, baadhi ya ndugu wa majeruhi wamelalamikia kuzuiwa kumuona ndugu yao na kutakiwa kuonesha vitambulisho.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger