Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » Jeshi la polisi lawaonya wananchi dhidi ya matumzi mabaya ya Silaha....

Jeshi la polisi lawaonya wananchi dhidi ya matumzi mabaya ya Silaha....

tangazo
 
JESHI la Polisi nchini limetoa onyo kali kwa watu wanaotumia vibaya silaha walizomilikishwa. 

Onyo hilo lilitolewa jana na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Advera Senso, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari na kuwataka watu hao kuacha mara moja tabia hiyo na badala yake wazingatie sheria na masharti waliyopewa wakati wa umilikishwaji.
 
Alisema kutokana na kushamiri kwa vitendo hivyo katika jamii,  jeshi hilo linaanza operesheni kali ya kuwabaini wote wanaofanya vitendo hivyo, ikiwa ni pamoja na kuwanyang’anya silaha hizo kwa wale watakaobainika kwenda kinyume cha sheria na matumizi ya silaha zao.
 
“Katika siku za hivi karibuni, imebainika baadhi ya watu waliomilikishwa silaha kihalali wamekuwa wakitumia silaha hizo kinyume cha malengo mazuri ya umilikishwaji.
 
Baadhi yao wamekuwa wakitoa vitisho kwa wananchi kwa kutumia silaha hizo bila sababu za msingi wawapo katika maeneo mbalimbali, kama vile kwenye mabaa, kumbi za starehe na hata kulipizana visasi, jambo ambalo ni kinyume cha sheria na malengo ya umilikishwaji.
 
“Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wote wazalendo na wenye mapenzi mema na nchi yetu kutoa taarifa zitakazosaidia kuwabaini  watu wanaojihusisha na vitendo hivyo, ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,” alisema Advera katia taarifa yake hiyo.
 
Alisema wananchi wanaweza kutoa taarifa kupitia namba ya simu 0754785557 pamoja na namba za simu za makamanda wa mikoa au kwenye kituo chochote cha Polisi.

TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger