tangazo
MAJERUHI Francis Shumira aliyejeruhiwa katika tukio la kushambuliwa kwa risasi Ilala Dar es salaam juzi amefariki dunia jana asubuhi Hospitali ya Muhimbili alikolazwa MOI kwa matibabu.
Kufariki kwa Francis kunafanya idadi ya watu watatu waliofariki katika tukio
hilo hadi hivi sasa huku ikiacha majeruhi wawili ambao ni Christina Alfred
Newa Mwanafunzi wa masuala ya Mawasiliano visiwa vya Syprus na mama
mzazi wa Christina, Hellen Elieza Newa.
Familia imekiri kuwa Christina na Marehemu Munisi walikuwa na mahusiano
lakini ni zamani na walitengana kutokana na vurugu alizowahi mfanyia
siku za nyuma.
Taarifa za Polisi zinapasha kuwa, Watu walio poteza maisha
katika tukio hilo ni
Gabriel Munisi ambaye aliwapiga risasi wenzake na kisha kujiua mwenyewe , Alfa
Alfred ambaye ni mdogo wake Christina , na Francis Khiranga Shumira ambaye amefariki jana akiwa Muhimbili