Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » Makamu wa Rais Dr. Bilal awaoongoza wananchi kuuaga mwili wa Dr. Sengondo Mvungi jijini Da es Salaam leo

Makamu wa Rais Dr. Bilal awaoongoza wananchi kuuaga mwili wa Dr. Sengondo Mvungi jijini Da es Salaam leo

tangazo

Jeneza lenye mwili wa marehemu Dkt.Sengondo Mvungi, likiwasili kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo kwa ajili ya kuagwa
 Jeneza likipelekwa sehemu iliyoandaliwa
 Mashada ya maua na picha ya marehemu
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza kutoka salamu za rambi rambi za serikali wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi,kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Katiba Jaji Joseph Sinde Warionba akiongea machache wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi,kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.

 Makamu wa Rais Dkt Gahlib Bilali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Katiba Jaji Joseph Warioba, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Mhe Angela Kairuki na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mhe James Mbatia wakiwa katika shughuli za kuaga mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi,kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo. 
Misa wakati wa shughuli hiyo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuagwa mwili huo iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda  akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuagwa mwili huo iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo. 
Picha na OMR
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger