tangazo
Hali ya wanawake inazidi kuwa mbaya ndani ya nchi yao TANZANIA inayosifiwa kuwa ni Kisiwa cha Amani ...
Tukio hili lilitokea mapema mwezi wa nane
mwaka huu Kijiji cha Nyantira Tarime Mara. Katika mazungumzo yake, binti
HUYU alisema kwamba anatamani sana kurudi nyumbani kwa wazazi wake, tatizo ni kwamba
kwa kuwa alilipiwa MAHARI na mume wake (aliyemkata panga mguu na kuutoa) hawezi
kurudi kwao , wala mama yake hawezi kumkubalia arudi kwao ni mpaka baba yake
aje atoe ruhusa ya yeye kurudi nyumbani au abaki kwa mume wake....
Samahani
kwa picha mbaya, lakini hatuna budi kuonyesha unyama uliopita kipimo ambao
wanawake wanaupitia. Na huu ni mfano halisi kwa mwanamke huyu wa Tarime Musoma.
Picha ya juu ni kipande cha mguu wa huyo binti ambao mume alipitisha panga
mithili ya mtu anayekata muwa, picha inaonyesha mguu uliobaki na mguu wa kushoto pia
ulikatwa lakini haukutoka, pamoja na mkono wake wa kushoto ulikatwa lakini
haukutoka.
Mama
mzazi wa binti aliyekatwa mguu na mkwe wake akilia kwa uchungu mkubwa alipokuwa
anaelezea kisa kilichomkumba binti yake.
Ni huzuni kubwa sana ukivaa viatu vya
familia hii. Mama anasema kwa utamaduni wao baba wa mtoto aliyekatwa yaani mume
wake ndiye mwenye dhamana ya kuamua mtoto arudi nyumbani au aendelee kubaki kwa
mume fedhuli aliyemgeuza mwenzake ni pingili la muwa au kitoweo Bucher.
Juu ni
mama na chini ni binti akiwa na mawazo juu ya kupoteza mguu wake kwa sababu tu
mume kaamua kuukata.
-credit
wanawake live tv




