Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » Mume amshitaki mke wake kwa kumzalia watoto wenye sura mbaya, ashinda kesi na kulipwa tsh.192, 840,000/=

Mume amshitaki mke wake kwa kumzalia watoto wenye sura mbaya, ashinda kesi na kulipwa tsh.192, 840,000/=

tangazo

Mwanaume wa China ameshinda kesi ya kulipwa $120 000 ( tsh.192, 840,000/=) baada ya kumpa taraka mke wake kwa kumzalia watoto wabaya.
 
Awali, mwanaume huyo aitwaye Jian Feng, alikuwa akimtuhumu mke wake kuwa anatoka nje ya ndoa kwakuwa haikuwa ikimuingia akilini kuzaa watoto wasiovutia kama wao..
 
Baada ya DNA kuweka bayana kuwa kweli watoto ni wa kwake, mke wa Feng aliamua kuitoa siri nyingine ndogo.

Kabla ya wanandoa hao kukutana, mke wa Feng alikuwa amefanyiwa upasuaji wa urembo (cosmetic surgery) uliogharimu $100,000 nchini Korea Kusini na ndio maana watoto waliozaliwa walikuwa tofauti na wazazi.
 
Feng alimshitaki mke wake kwa kuficha ukweli huo na kumfanya amuone mrembo. Kutokana na maelezo hayo, jaji alimpa ushindi Feng na kumwamuru mke wake amlipe fidia ya dola $120,000.
 
Akiongea na Irish Times, Feng alisema: “Nilimuoa mke wangu kwa upendo, lakini mara baada ya kupata mtoto wa kwanza tulianza kuwa na migogoro. Binti yetu alikuwa mbaya haswaa, hadi kufikia wakati akawa ananitisha.”
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger