tangazo
SEXY lady wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amesheherekea
mwaka mmoja na wenzake tangu alipoacha kutumia madawa ya kulevya ‘unga’.

Wikiendi iliyopita Ray C alitupia picha kwenye ukurasa wake wa
mtandao wa kijamii wa Instagram zilizomuonesha akiwa na wenzake katika
Hospitali ya Mwananyamala, Dar ambako huwa wanapata dozi ya madawa ya
kulevya.

Aliandika: “Nawapenda sana hawa wenzangu wote, tuligundua tatizo
tukasaidiwa na sasa tumepona na tunamshukuru Mungu...Tanzania bila
madawa ya kulevya inawezekana.”
