Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Showing posts with label WASTARA. Show all posts
Showing posts with label WASTARA. Show all posts

"WANAUME WALIO MSAIDIA SAJUKI WAMENIGEUKIA NA KUNITAKA KIMAPENZI"-WASTARA JUMA


Wastara Juma amefunguka kuwa wanaume wengi waliokuwa wakimsaidia wakati mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ akiwa mgonjwa wanamgeuka na sasa wanamtaka kimapenzi.

Akizungumza kupitia Kipindi cha Take-One katika Runinga ya Clouds chini ya Zamaradi Mketema, Wastara alisema baadhi ya watu ambao walikuwa karibu naye wakati Sajuki anaumwa sasa hivi wamegeuka na kumtaka kimapenzi, jambo ambalo linamuumiza na kumshangaza mno.

Bishosti huyo alisema kuwa tofauti na wanaume hao ambao walikuwa wakimpa sapoti kipindi hicho, bado wapo wengine kibao kutoka nje na ndani ya nchi ambao wanatuma maombi kwake lakini anawaona wote ni matapeli na wanamtamani tu hivyo hayupo tayari kuingia kwenye uhusiano wa aina hiyo.

“Kweli ninaumia sana kwa sababu ninakaa na kujiuliza hawa wanaume walikuwa wanasubiri mume wangu afariki dunia ndiyo wanitongoze?
 

“Kusema kweli inanishangaza, hata watu ambao sikuwadhania kabisa eti nao wananitaka, watu wajue kwa sasa sipo tayari kuwa na mwanaume.
 

“Sitaki kukurupuka kwa sababu naweza nikaingia kwenye shimo la taka kwani jamii itanikimbia kutokana na kunuka, natamani kumpata mwanaume anayefanana na mume wangu kitabia.

“Uvumilivu wangu na uzuri ulitokana na kutunzwa siyo aje mtu anayetaka nikavumilie shida, hilo sitaki litokee, namuomba Mungu sana,” alisema Wastara.
TUPE MAONI YAKO

WASTARA JUMA AANZA KUSAKA MUME WA KUMUOA BAADA YA KIFO CHA MUMEWE

 
STAA wa filamu za Kibongo, Wastara Juma amesema hana haraka ya kuolewa kwani anahitaji mume na si mwanaume  wa kupita

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Wastara alisema kwa sasa yupo huru kutoka na mtu yeyote ampendaye kutokana na sheria na dini inavyosema ila kwa sasa shughuli za kuigiza zimembana.
 

‘Nahitaji mume na si mwanaume  wa kupita,  awe mvumilivu, mchapakazi pia awe na hofu ya Mungu. Kwa sasa nafanya filamu zangu kama kumuenzi marehemu mume wangu,” alisema Wastara.
TUPE MAONI YAKO

FILAMU ALIYOIGIZA SAJUKI NA WASTARA YAINGIA SOKONI....




Filamu aliyoigiza marehemu Sajuki na mke wake Wastara ‘Kivuli’ leo imeingia sokoni rasmi. Filamu hiyo iliyotayarishwa na Wajay Film Co na kusambazwa na kampuni ya Steps imewahusisha pia waigizaji Slim Omary na Mohammed Said.
TUPE MAONI YAKO

"MUME WANGU ALINIPENDA SANA JAMANI..NITAISHIJE MIMI...??" ...HAYA NI MANENO YA WASTARA YALIYOWALIZA WENGI

MKE wa aliyekuwa mcheza filamu mahiri Bongo, marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’, Wastara Juma amesema kuwa, gari na nyumba vitamuumiza maishani kwa kuwa ndivyo vitakavyomkumbusha uwepo wa marehemu.

Akizungumza huku akilia kwenye msiba wa mumewe nyumbani kwake, Tabata-Bima, Dar, Wastara alisema yeye na Sajuki waliishi kama mapacha na kila walipokuwa wakitaka kutoka walikuwa pamoja na mara nyingi marehemu ndiye aliyekuwa akipenda kuendesha gari hilo kila walipokuwa wakienda. 


“Japokuwa alikuwa akiumwa lakini alipenda aendeshe gari yeye huku akisema mimi nina tatizo la mguu. Mume wangu alinipenda sana jamani, alijitolea kuumia zaidi kwa ajili yangu, nitaliangaliaje hili gari jamani,” alisema Wastara huku akibembelezwa na waombolezaji.

 Wastara aliwatoa chozi watu pale aliposema, marehemu alikuwa na kawaida ya kumwambia yeye ni malkia hivyo alitakiwa aendeshwe badala ya kuendesha.


“Sajuki alikuwa akiniambia mimi ni malkia wa nyumba, sitakiwi kuendesha gari, alisema natakiwa kuendeshwa, oooh jamani, nitaishije kwenye hii nyumba mimi,” alisema Wastara huku akizidi kulia.


Sajuki alifariki dunia alfajiri ya Jumatano iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wodi ya Mwaisela kutokana na ugonjwa wa saratani ya ngozi pamoja na uvimbe tumboni. 


Alizikwa jana katika Makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam. Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina.
TUPE MAONI YAKO
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger