Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Showing posts with label sajuki. Show all posts
Showing posts with label sajuki. Show all posts

FILAMU ALIYOIGIZA SAJUKI NA WASTARA YAINGIA SOKONI....




Filamu aliyoigiza marehemu Sajuki na mke wake Wastara ‘Kivuli’ leo imeingia sokoni rasmi. Filamu hiyo iliyotayarishwa na Wajay Film Co na kusambazwa na kampuni ya Steps imewahusisha pia waigizaji Slim Omary na Mohammed Said.
TUPE MAONI YAKO

HISTORIA FUPI YA MAREHEMU SAJUKI NA CHANZO CHA MAUTI YAKE...


KAMA ilivyo kawaida ya maisha ya binadamu, kuna kupanda na kushuka. Katika maisha ya aliyekuwa staa wa filamu za Kibongo, marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ alipanda na kushuka na alipitia katika raha na shida ambazo ndizo zilikuwa nyingi. 

HISTORIA
Sajuki alizaliwa Aprili 4, 1986 mkoani Songea na kupata elimu ya msingi katika Shule ya Mfanyakazi, Manispaa ya Songea kuanzia mwaka 1995 hadi 2001. 


Mwaka 2002 alijiunga na shule ya Sekondari ya Jeshi Ruhuwiko ambayo nayo ipo Manispaa ya Songea hadi alipohitimu kidato cha nne mwaka 2005.

MISHEMISHE ZA KUCHOMOKA KIMASHA DAR
Mwishoni mwa mwaka 2005, Sajuki aliingia rasmi jijini Dar es Salaam na kuanza kwa kufanya biashara ndogondogo ambapo mwaka huohuo alianza kusaga soli akiomba kuingia kwenye Kundi la Sanaa la Kaole.


Pamoja na changamoto kibao lakini hakukata tamaa. Alifanikiwa na akaonesha kipaji kwenye michezo mbalimbali iliyokuwa ikirushwa katika Kituo cha Runinga cha TVT (kwa sasa TBC1).


AINGIA KWENYE FILAMU
Baada ya kuonekana kwenye michezo kadhaa akiwa Kaole, Sajuki aliingia kwenye uchezaji wa filamu ambapo ya kwanza kuonekana ni ile ya Revenge aliyoshirikishwa na mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’.


Hakuishia hapo, baada ya filamu hiyo aliendelea kusaka mingo za filamu ambapo ya pili ni ile ya Victoria. Kabla hajakaa vizuri akakutana na mwigizaji Deogratius Shija ambaye alimpa shavu kwenye Two Brothers na nyingine nyingi. 


Safari ikaanza, zikafuata nyingine za Mboni Yangu, Shetani wa Fedha, Vita, The Killer, Round, Kozo Pata, Mchanga, Brifcase na ya mwisho ni Kivuli aliyocheza akiwa anaumwa.

SHIJA AMKUTANISHA NA WASTARA
Mwaka 2008, Shija aliwakutanisha Sajuki na mkewe Wastara kwenye filamu ya Two Brothers ambapo huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa uhusiano wao mpaka kuja kuoana.


Mwaka 2009, wawili hao walifunga ndoa ikiwa ni miezi kadhaa tangu Wastara akatwe mguu kutokana na ajali ya pikipiki waliyoipata wakiwa pamoja wakati wa uchumba.
Siyo siri, ndoa yao imekuwa mfano wa kuigwa na jamii pamoja na mastaa wenzao kwani walikuwa wanapendana kupindukia.


KUUGUA
Sajuki alianza kuugua tangu mwaka 2011 ambapo alitibiwa katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam. Baada ya hali kuwa mbaya alihamishiwa Muhimbili na kugundulika kuwa alikuwa na uvimbe tumboni.


Baada ya uchunguzi huo, mwaka 2012 alipelekwa India kwa ajili ya matibabu ambapo alifanyiwa uchunguzi upya na kugundulika kuwa ana ugonjwa wa saratani ya ngozi, uvimbe tumboni na upungufu wa damu. 


Alipewa dawa za kutumia kwa miezi kadhaa na kuambiwa arejee tena lakini mauti yamemkuta akiwa kwenye maandalizi ya kurudi India.

Sajuki alifariki Januari 2, mwaka huu katika Hospitali ya Muhimbili na ameacha mjane na mtoto mmoja mwenye umri wa miezi kumi aitwaye Farheen.


Credit:GPL
TUPE MAONI YAKO

"MUME WANGU ALINIPENDA SANA JAMANI..NITAISHIJE MIMI...??" ...HAYA NI MANENO YA WASTARA YALIYOWALIZA WENGI

MKE wa aliyekuwa mcheza filamu mahiri Bongo, marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’, Wastara Juma amesema kuwa, gari na nyumba vitamuumiza maishani kwa kuwa ndivyo vitakavyomkumbusha uwepo wa marehemu.

Akizungumza huku akilia kwenye msiba wa mumewe nyumbani kwake, Tabata-Bima, Dar, Wastara alisema yeye na Sajuki waliishi kama mapacha na kila walipokuwa wakitaka kutoka walikuwa pamoja na mara nyingi marehemu ndiye aliyekuwa akipenda kuendesha gari hilo kila walipokuwa wakienda. 


“Japokuwa alikuwa akiumwa lakini alipenda aendeshe gari yeye huku akisema mimi nina tatizo la mguu. Mume wangu alinipenda sana jamani, alijitolea kuumia zaidi kwa ajili yangu, nitaliangaliaje hili gari jamani,” alisema Wastara huku akibembelezwa na waombolezaji.

 Wastara aliwatoa chozi watu pale aliposema, marehemu alikuwa na kawaida ya kumwambia yeye ni malkia hivyo alitakiwa aendeshwe badala ya kuendesha.


“Sajuki alikuwa akiniambia mimi ni malkia wa nyumba, sitakiwi kuendesha gari, alisema natakiwa kuendeshwa, oooh jamani, nitaishije kwenye hii nyumba mimi,” alisema Wastara huku akizidi kulia.


Sajuki alifariki dunia alfajiri ya Jumatano iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wodi ya Mwaisela kutokana na ugonjwa wa saratani ya ngozi pamoja na uvimbe tumboni. 


Alizikwa jana katika Makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam. Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina.
TUPE MAONI YAKO

MBUNGE WA KINONDONI AAHIDI KUISAIDIA FAMILIA YA SAJUKI


Kutokana na hali ya majonzi na masikitiko makubwa kwenye familia ya  marehemu Sajuki mbunge wa Kinondoni Iddi Azam ameahidi kuisaidia kwa hali na mali familia aliyoiacha marehemu Sajuki

Ahadi hizo alizisema juzi wakati alipofika nyumbani kwa marehemu kwa lengo la kutoa pole na salamu za rambirambi kwenye familia hiyo

Azam alisema kuwa anadeni kubwa kwenye familia hiyo pamoja na  mtoto aliyeachwa na marehemu, hivyo ni wajibu wake kumsaidia kadri ya uwezo wake

"Kila mtu anaiona hali ya Wastara sasa ilivyo basi sisi tulio baki tuwe kama Sajuki, kwani mapenzi walio kuwa nayo ni mfano wa kuigwa kwetu, hivyo nina jukumu la kuisaidia familia hii" alisema Azam

Aliongezea kuwa ni jukumu la kila mmoja wao kumuenzi marehemu Sajuki kwa vitendo Sajuki anazikwa leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam
TUPE MAONI YAKO

RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WAENDA KUTOA POLE NYUMBANI KWA MAREHEMU SAJUKI LEO....


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko ' Sajuki' nyumbani kwao wafiwa Tabata Bima jijjini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko ' Sajuki' nyumbani kwao wafiwa Tabata Bima jijjini Dar es salaam leo Januari 4, 2013. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko ' Sajuki' Tabata Bima jijjini Dar es salaam leo ambako walienda kutoa pole leo Januari 4, 2013
TUPE MAONI YAKO

PICHA ZA RAIS KIKWETE ALIPOONGOZA MAZISHI YA SAJUKI LEO..



Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) likiwasili kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam mchana huu tayari kwa Mazishi yaliyoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na baba mzazi wa marehemu Sajuki  wakati wa mazishi ya msanii huyo  leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la marehemu Sadick Juma Kilowoko 'Sajuki' leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye Kaburi la Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika mchana kwenye Makaburi ya Kisutu,Jijini Dar es Salaam.
TUPE MAONI YAKO

MWILI WA MAREHEMU SAJUKI UMEKWISHA ZIKWA......MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI



 Sehemu ya waliohudhuria msiba wa Sajuki katika makaburi ya Kisutu 
Wadau mabali mbali wakisubiria mwili wa Marehemu Sajuki, huku Profesa Jay akionekana kwa mbali miongoni mwa wanaousubiri mwili.
Umati wa watu ukiwa makaburini Kisutu Dar
 Mwili wa marehemu Sajuki ukiwasili katika makaburi ya Kisutu tayari kwa mazishi
  Hapa ndipo sajuki amelala! May his soul R.I.P


TUPE MAONI YAKO

HII NDO SAFARI YA MWISHO YA MAREHEMU SAJUKI...

 Waombolezaji wa Msiba wa Msanii wa Filamu hapa nchini,Marehemu  Sadick Juma Kilowoko wakibeba jeneza lenye mwili wake tayari kwa taratibu za kwenda Mazikoni,wakitokea Nyumbani kwa Marehemu Tabata Bima.

Sasa hivi mwili wa Marehemu upo katika Msikiti wa Sheahk Adhir,Kariakoo kwa ibada ya Kusalia Mwili na baada ya Swala ya Ijumaa,Mwili utazikwa kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mwili ukipakiwa kwenye gari.
Dua ikisomwa kabla ya kuondoka na Mwili wa Marehemu kwenda mazikoni.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania,Saimon Mwakifwamba akimpokea Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe alipokuwa akiwasili msibani hapo.
Waombolezaji wakiwa Msibani mapema asubuhi hii.
Pamoja na kwamba kulikuwa na Mvua kubwa lakini hakuna alitaka kuondoka msibani hapo mpaka pale mwili ulipoondoka kuelekea Msikitini kwa Kusalia na baadae kwenye Mazishi.
Mwili ukiondoka nyumbani.
TUPE MAONI YAKO

MWILI WA MAREHEMU SAJUKI UNAELEKEA MSIKITINI KWA MAOMBEZI YA MWISHO


 
Kwa wale mliokuwa mnataka kuja nyumbani kwa marehemu ndio tunaenda kusalia maiti msikitini mjini kisha tunaenda kuzika makaburi ya kisutu
TUPE MAONI YAKO

TASWIRA MBALIMBALI TOKA NYUMBANI KWA MAREHEMU SAJUKI....



Mazishi ya msanii mahiri wa tasnia ya filamu Juma Issa Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia juzi yanatarajiwa kufanyika leo mchana katika makaburi ya Kisutu baada ya sala ya Ijumaa. 

Akiongea na mtandao huu, mwenyekiti wa kamati ya mazishi Steve Nyerere amesema kuwa msiba huu unasimamiwa na shirikisho na wasanii wa filamu na wadau wa tasnia hiyo.

Kamati ya mazishi ikiteta jambo na  Kiongozi wa shilikisho la filamuKamati ya mazishi ikiteta jambo na Kiongozi wa shilikisho la filamu
Stive Nyerere akipokea mchango wa mazishi kutoka chuo cha filamu cha Pastor MyambaStive Nyerere akipokea mchango wa mazishi kutoka chuo cha filamu cha Pastor Myamba
Wasanii wa filamu wakiwa wamekaa kimya wakisikiliza jambo kutoka kwa Uongozi wa shilikisho la FilamuWasanii wa filamu wakiwa wamekaa kimya wakisikiliza jambo kutoka kwa Uongozi wa shilikisho la Filamu
Kiongozi wa shilikisho la filamu akitoa mawili matatu kwa wasanii wa filamuKiongozi wa shilikisho la filamu akitoa mawili matatu kwa wasanii wa filamu
Mdau akitoa mchango wa mazishiMdau akitoa mchango wa mazishi
Mdau akitoa mchango wa mazishiMdau akitoa mchango wa mazishi

Waigizaji wakiwa na uzuni
Viongozi wa kamati ya mazishi wakijaliana jambo na wadau wa filamuViongozi wa kamati ya mazishi wakijadiliana jambo na wadau wa filamu
Mdau wa filamu akitoa pole na kuwafariji ndugu wa marehemuMdau wa filamu akitoa pole na kuwafariji ndugu wa marehemu
Waigizaji wa filamu wakiwa wamekaa kwa uzuniWaigizaji wa filamu wakiwa wamekaa kwa huzuni
wasanii wa filamu wasanii wafilamu
Baadhi ya wasanii wakiwa katika pozi la uzuniBaadhi ya wasanii wakiwa katika pozi la uzuni
Waigizaji wa filamuWaigizaji wa filamu

TUPE MAONI YAKO

RATIBA KAMILI YA MAZISHI YA MAREHEMU SAJUKI....

HII NDO RATIBA RASIMI YA MAZISHI YA SAJUKI...

TUPE MAONI YAKO

MWILI WA SAJUKI WAHAMISHIWA MSIKITINI HUKU MAANDALIZI YA MAZISHI YAKIENDELEA

MWILI msanii nyota wa filamu, Juma Kilowoko “Sajuki” aliyefariki juzi alfajiri, umeondolewa katika vyumba vya kuhifadhia maiti vya Hospital ya Taifa, Muhimbili.

Na badala yake, mwili wa Sajuki sasa umekwenda kuhifadhiwa katika chumba cha maiti cha msikiti wa Shadhir (Masjid Shadhully) uliopo Kariakoo mtaa wa Sikukuu na Twiga.

Msanii Issa Mussa “Cloud” aliiambia mpekuzi kuwa lengo la kuhamisha mwili huo ni kujaribu kufanikisha taratibu zote za kesho kwenda na muda.

“Muhimbili process za kuchukua mwili ni ndefu na hata huduma zao za kuosha mwili wa marehemu ni ndefu pia kutokana na wingi wa maiti zinahofadhiwa na kuoshwa hospitalini hapo.

“Hivyo tumeona tuupeleke mwili Masjid Shadhully kwa vile hakuna msongamano kama wa Muhimbili” alisema Cloud. 
 
Masjid Shadhully ndio msikiti atakaoswaliwa Sajuki ambapo mwili wake utachukuliwa msikitini hapo saa 4 asubuhi na kupelekwa nyumbani kwake Tabata na baadae kurudishwa tena Masjid Shadhully kwa ajili ya kuswaliwa na kwenda kuzikwa makaburi ya Kisutu baada ya swala ya Ijumaa saa 7 za mchana.
 
MAANDALIZI  YA MSIBA

Wasanii wa filamu Mike Sangu (kushoto) Jacob Steven ‘JB’ (katikati) na Denes Sweya ‘Dino’ wakipanga mikakati msibani hapo.
Mke wa marehemu Sajuki, Wastara Juma ‘Stara’, aliyejifunika akifarijiwa na waombolezaji.

JB akimpa pole mama yake mzazi Sajuki
Stara akiwa katika maombolezo.
JBakijiweka tayari kwa shughuli za msibani.

Baba wa marehemu Sajuki, mzee Kilowoko, akimsikiliza JB.

MAANDALIZI ya kumzika msanii wa filamu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ yanaendelea nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam.

Habari za kuaminika ni kwamba Sajuki atazikwa kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo saa  mchana.
TUPE MAONI YAKO
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger