Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » , » MSANII WA MCHIRIKU ''OMARI OMARI'' AFARIKI DUNIA NA ATAZIKWA KESHO

MSANII WA MCHIRIKU ''OMARI OMARI'' AFARIKI DUNIA NA ATAZIKWA KESHO

tangazo

MSANII nyota wa miondoko ya Mchiriku, Omari Omari, aliyefariki leo afajiri atazikwa kesho saa 7 mchana. Kwa mujibu wa King Sapeto, rafiki wa karibu wa marehemu, mazishi yatafanyika Temeke Mikoroshini jijin iDar es Salaam na kuanzia leo ndugu na jamaa wa marehemu wanategemea ujumbe mzito kutoka kwa viongozi wa Serikali watakaopishana kwenda kutoa mkono wa faraja kwenye nyumba ya msiba.
Kwa siku za hivi karibuni viongozi wa serikali na vyama mbali mbali vya siasa wamekuwa mstari wa mbele kwa kushiriki bega kwa bega kwenye misiba ya wasanii, hivyo watu wa karibu na Omari Omari wanategemea hali hiyo pia itatokea kwa ndugu yao kipenzi. "Hatutegemi ubaguzi wa misiba" anaeleza mmoja wa ndugu wa marehemu.
 
Omari Omari aliyetamba na wimbo “Kupata Majaaliwa” ndani yake kukiwa na mstari mkali unaosema ndefu amekosa ng’ombe lakini mbuzi kapewa, alifariki katika hospitali kuu ya Temeke baada ya kuugua ugonjwa wa kifua kikuu.
Msiba uko Temeke Mikoroshini nyumbani kwa baba yake. 

MUNGU AMLAZE MAHALA PEMBA PEPONI- AMINA
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger