tangazo
Kama
unakerwa na tabia za mapedeshee wapenda sifa kwa kutajwa kwenye nyimbo
za muziki wa dansi na kumwaga hela ukumbini, hauko peke yako. Jacqueline
Wolper naye humchefua.
“Napenda kutumia fursa hii leo kuzungumza kitu fulani kidogo tu ambacho nimekiona mimi,” ameandika Wolper kwenye blog yake.
“Napenda kutumia fursa hii leo kuzungumza kitu fulani kidogo tu ambacho nimekiona mimi,” ameandika Wolper kwenye blog yake.
“Mara nyingi
nimekua nikisikia kwenye nyimbo nyingi za wanamuziki wa Tanzania hata
wa maeneo mbali mbali kama Jamhuri ya watu wa Congo wakiwataja watu
flani flani ambao inaaminika na watu wenye kipato kikubwa kifedha au
huwa wanawasaidia kimuziki hata kimaisha wakati mwingine.
Kinachonishangaza kwanini wanapenda kuwatunza kwenye majukwaa tuu?
Hao wanaojiita mapedeshee wanaopenda kutajwa kwenye nyimbo za hao
wasanii. Nawaomba mapedeshee waende kwenye vituo vya kulea watoto yatima
na kutoa misaada ya kifedha na Inshalah Mwenyezi Mungu atawazidishia.”