tangazo
Mahakama
ya Uhalifu wa Kmataifa ya Bangladesh imemhukumu adhabu ya kifo kiongozi
wa kiislamu Delwar Hossain Sayedee, baada ya kumkuta na hatia ya
uhalifu dhidi ya ubinadamu, alioutenda wakati wa vita vya kupigania
uhuru mwaka 1971.
Sayedee
ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa chama cha Jamaat-e-Islami wakati
huo, alikuwa akituhumiwa kuamuru mauaji ya halaiki, ubakaji na mateso
mengine yaliyofanywa wakati wa vita hivyo.
Wakili wake amesema kesi dhidi ya mteja wake ilikuwa na ushawishi wa kisiasa na imekiuka kwa kiasi kikubwa maadili ya haki.
Watu zaidi ya 20 wamekufa katika ghasia zilizofuatia kutolewa kwa hukumu hiyo.