TAIFA STARS YAIPA KIPIGO CHA 3-1 MOROCCO
tangazo
Taifa Stars imefanya kile Watanzania walichowatuma baada ya kuwalaza
Simba wa Atlas kwa mabao matatu kwa moja.
Kipindi cha kwanza Stars
walicheza kandanda la kuvutia na kupoteza nafasi nyingi za wazi huku
Mbwana Samatta akionekana kuwa mwiba mkali kwa beki ya Morocco muda
wote.
Katika kipindi cha pili, Thoma Ulimwengu akitokea benchi alifunga
bao la kwanza baada ya kuunganisha mpira wa kona, Dakika ya 66 ilikuwa
ni Mbwana Samatta ambaye alimchambua golikipa wa Morocco na kufunga bao
la pili na kuongeza bao la tatu katika ya 80.
Stars iliendelea
kushambulia kwa kasi huku ikigonga mwamba mara mbili. Dakika ya 90
Morocco ilipata bao la kufutia machozi na hivyo mchezo kuisha kwa 3-1.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK