tangazo
Dar es Salaam.
Kuporomoka jengo lililopo Mtaa wa Indira Gandhi Jijini Dar es Salaam, huenda ikawa mwanzo tu wa kuporomoka majengo mengine zaidi hasa kufuatia matokeo ya tume iliyoundwa mwaka 2006 iliyobaini zaidi ya majengo 100 Jijini Dar es Salaam yamejengwa bila kuzingatia viwango.

Kwanini
Serikali haichukui hatua kwa majengo hayo 100 yaliyobainika kuwa
hayajajengwa kwa kuzingatia viwango? Wenye akili timamu wanaweza
kuendelea kujiuliza maswali mengi zaidi na kujibu wanavyoweza.
Wapo
wanaoweza kusema rushwa ndio inasababisha mambo mengi kutofanyiwa kazi
kwa ufasaha, lakini mbele ya sheria utaombwa utoe ushahidi, hapo bila
shaka patafanya wengi kubadili maneno kwamba aaah labda Serikali
inaendelea kufanya mchakato, mpango mkakati, mkakati yakinifu nk dhidi
ya majengo hayo
.
Kubomoa
jengo lenye ghorofa 16 au hata chini au zaidi ya hapo baada ya
kulibaini halijazingatia viwango, ni lazima uwe na uso mgumu. Baadhi ya
wananchi wanasema wenye majengo bila shaka hawawezi kutulia wakisubiri
sheria ifanye inachotakiwa kufanya, hapo ndipo ugumu unapoanzia.
Pinda analo na kujibu
Baadhi ya watu wanafikiri kuondolewa madarakani kwa viongozi walio katika wizara husika na sakata hili akiwemo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye ofisi yake ilichunguza na kubaini maghorofa zaidi 100 kuwa ni feki, kunaweza kuwa ni mojawapo ya mambo muhimu kwa sasa.

Mke na watoto wafukiwa
Licha kwamba jengo hilo liliporomoka saa 2.30 asubuhi, baadhi ya watu waliofukiwa na kifusi cha jengo hilo walikuwa wakiwasiliana na jamaa zao kwa njia ya simu na wengine wakipiga kelele za kuomba msaada.

Idd
Baka ambaye alikuwa akiwasiliana na mkewe ambaye aliegesha gari huku
ndani kukiwa na watoto wake wawili alikwenda dukani kununua bidhaa, mara
jengo hilo likaporomoka, alikuwa akiwasiliana nae hadi majira ya mchana
simu ya mke wake haikuwa inapatikana.
Vifaa duni
Ni dhahiri kwamba endapo kungekuwapo na vifaa vya kutosha katika zoezi la uokoaji lingewezaa kufanikiwa kwa muda mfupi na kwa kiasi kikubwa hivyo kuwapata majeruhi wakiwa hai.
Ni dhahiri kwamba endapo kungekuwapo na vifaa vya kutosha katika zoezi la uokoaji lingewezaa kufanikiwa kwa muda mfupi na kwa kiasi kikubwa hivyo kuwapata majeruhi wakiwa hai.
Katapila latumika
Cha ajabu na aibu kwa taifa kutokuwa tayari kwa kuwa na vifaa vya kuokolea kwani tangu saa 2:30 hadi ilipofika saa 4.30 ndipo lilipatikana katapila moja ambalo nalo halikuwa na tija kutokana na kuwapo kwa uwezekano wa kuwakandamiza au kuwajeruhi zaidi watu waliofukiwa na kifusi hicho.

Kutokana
na kutokuwepo na vifaa vya kukatia nongo waokoaji iliwachukua takribani
dakika 15 kukata nondo zilizokuwa zimemkandamiza.
Umati
wa watu ulivamia kifusi na kuanza kukisomba kwa mikono ili hali jambo
hili lilikuwa kama mchezo wa kuigiza ambao umegharimu uhai wa watu zaidi
ya 35 pamoja na kuharibu magari yaliyobondwa na kuwa kama chapati
takribani matano.
Mashuhuda
Ali Mparang’ombe mmoja wa mafundi wa jengo hilo anasema kudondoka kwa jengo hilo ni mtiririko wa majengo mengine kutokuwa katika viwango vinavyotakiwa.
Ali Mparang’ombe mmoja wa mafundi wa jengo hilo anasema kudondoka kwa jengo hilo ni mtiririko wa majengo mengine kutokuwa katika viwango vinavyotakiwa.
“Ndugu
yangu mimi ni fundi nilikuwa nimeingia ndani, lakini nilitoka kwenda
upande wa pili kutafuta chai kwani leo (Ijumaa iliyopita) ni sikukuu
mama lishe hawakuwepo wengi hapa”anasimulia Mparang’ombe na kuongeza:
“Ndipo
kwa kule nilisikia kishindo kikubwa, kuja kuangalia ni jengo nililotoka
takribani dakika 15 tu limeanguka, nimepoteza watu muhimu sana ambao
tulikuwa tukifanya sote kazi, sasa sijui itakuwaje”.
Mparang’ombe
anasema jengo hilo lilikuwa likijengwa chini ya viwango kwani katika
ndoo 12 za mchanga walikuwa wakichanganya saruji mfuko mmoja.
Majengo mengi feki
“Hapa kama kama ndoo 12 mfuko mmoja wa saruji unategemea nini, na ni majengo mengi hapa mjini ambayo yamejengwa kwa aina hii, hivyo ni kudra za Mwenyezi Mungu zinahitajika”anasema Mparang’ombe.
“Hapa kama kama ndoo 12 mfuko mmoja wa saruji unategemea nini, na ni majengo mengi hapa mjini ambayo yamejengwa kwa aina hii, hivyo ni kudra za Mwenyezi Mungu zinahitajika”anasema Mparang’ombe.
“Jengo
hili lilipofika ghorofa ya 12 lilisimamishwa kujengwa na ghorofa ya 15
lilisimamishwa tena lakini hatujui alikuwa anatumia njia gani hadi akawa
anaruhusiwa kuendelea na ujenzi,” anasema.
Kibali cha jengo lililoanguka
Naibu Meya wa Halmashauri ya Ilala, Kheri Kessy alisema mwaka 2007 walitoa kibali kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa kushirikiana na ‘Aliraza Investment Limited’ kujenga jengo la ghorofa 10.
Naibu Meya wa Halmashauri ya Ilala, Kheri Kessy alisema mwaka 2007 walitoa kibali kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa kushirikiana na ‘Aliraza Investment Limited’ kujenga jengo la ghorofa 10.
Alipotakiwa
kueleza kwa nini hawakuchukua hatua baada ya kuendelea kujengwa hadi
kufikia ghorofa zaidi ya 10, alisema hawahusiki, ila kuna taasisi
zingine za Serikali zinazosimamia majengo zinatakiwa kuulizwa.
Matokeo ya tume yanapuuzwa
Mwaka 2006 Tume iliyoundwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa ilibaini kuwa zaidi ya maghorofa 100 yaliyopo jijini Dar es Salaam yalikuwa chini ya viwango.
Mwaka 2006 Tume iliyoundwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa ilibaini kuwa zaidi ya maghorofa 100 yaliyopo jijini Dar es Salaam yalikuwa chini ya viwango.
Idadi
hiyo ni tone tu la maghorofa yaliyo chini ya viwango nchi nzima ambayo
bila shaka kuyabomoa ugumu unakuja pale wamiliki wake kuwa vigogo na
wafanyabiashara mashuhuri.
Hali
kadhalika akiwa bungeni wakati wa majumuisho ya Ofisi yake Bungeni
mwaka 2008/09, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema ofisi yake ingechukua
hatua za makusudi dhidi ya majengo ili kuzuia vifo kama hivi visivyo vya
lazima. Kufumbia macho mambo ndiko leo kumesababisha watu zaidi ya 35
kuuawa, achilia mbali mali zingine yakiwemo magari.
Mwananchi