Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » , » AIBU: MREMBO ATUPWA JELA MIEZI 6 BAADA YA KUNASWA AKIJIUZA.....MCHUMBA WAKE AMWAGA MACHOZI HADHARANI

AIBU: MREMBO ATUPWA JELA MIEZI 6 BAADA YA KUNASWA AKIJIUZA.....MCHUMBA WAKE AMWAGA MACHOZI HADHARANI

tangazo


MREMBO Brandina Barthon (24), Jumatatu iliyopita alihukumiwa kwenda jela miezi 6 baada ya kupatikana na hatia kwenye kesi ya ukahaba iliyokuwa ikimkabili katika Mahakama ya Sokoine Drive (Jiji) jijini Dar.

Brandina alisomewa hukumu hiyo na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, William Mutaki ambaye alisema kutokana na ushahidi uliothibitika, mahakama hiyo inamhukumu kwenda jela miezi 6, ili liwe fundisho kwa wengine.

Hukumu hiyo ilimfanya mrembo huyo kuchanganyikiwa na kuangua kilio lakini mheshimiwa hakimu aliamua kukazia hukumu yake bila ya kupepesa macho.
 
Wakati mwanamke huyo akiangua kilio, afande wa Jeshi la Magereza alimfikia na kumchukua  kwa ajili ya kumpeleka kwenye Karandinga kuelekea Gereza la Segerea kuanza maisha ya jela.

Mbali na Brandina, mwanaume aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wa mtuhumiwa huyo aliyekuwa akifuatilia kesi hiyo naye alimwaga machozi baada ya kutolewa hukumu hiyo.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger