Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » "HAKUNA KANISA LILILOLIPULIWA KWA BOMU JIJINI DAR LEO"...HII NI KAULI YA KAMANDA KOVA

"HAKUNA KANISA LILILOLIPULIWA KWA BOMU JIJINI DAR LEO"...HII NI KAULI YA KAMANDA KOVA

tangazo
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kova amesema Taarifa zilizoenea kwamba Bomu limelipuka katika Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania (KKKT), Kunduchi jijini Dar es Salaam zimeenea ndivyo sivyo na kwamba askari walikuwa wanapambana na majambazi.


Wakati taarifa zikiwa zimesambaa katika mitandao ya kijamii na mitaani kwamba kuna kanisa la KKKT limeshambuliwa na bomu hivi punde, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kova amesema kwamba taarifa hizo sio za kweli na kwamba askari wa jeshi la polisi walikuwa wanapambana na majambazi karibu na eneo la kanisa hilo. 




Katika mapambano hayo polisi waliwarushia majambazi hayo bomu ili kuyakamata.

"Wakati askari wetu wanapambana na majambazi hayo- waumini wa kanisa hilo wamejitokeza kuwasaidia askari wetu. Naomba unisaidie kukanusha siyo kweli, nitazungumza na vyombo vingine vya habari kuweka sawa," amesema Kamanda Kova hivi Punde. 

TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger