Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » , » JESHI LA TANZANIA LIMESHATUA CONGO.....WAASI WA M23 WAANZA KUHAHA KWA KUJIKOSHA KWA WANANCHI

JESHI LA TANZANIA LIMESHATUA CONGO.....WAASI WA M23 WAANZA KUHAHA KWA KUJIKOSHA KWA WANANCHI

tangazo

Kwa mujibu wa mwandishi aliye na waasi  wa  m23, Diana Katabarwa kwenye Blog yake  anamnukuu kiongozi wa kisiasa wa M23  Mr. Bisimwa akiwambia wakazi wa North Kivu kuwa majeshi ya Tanzania na South Africa nimajeshi dhalimu yaliyo jaa rushwa na hayawezi kuibadili Congo....


Bisimwa anadai  kwamba  majeshi  ya  Tanzania  yamekuja kuiba mali na kumsaidia KABILA awatawale   hali  itakayosababisha   jeshi lake la FDLR na waasi wa MAI MAI wapewa nafasi ya kuwa pora mali zao na kuwabaka wake zao na watoto....

Mbali  na  hayo,  bwana Busimwa anadai kinyume na taarifa zilivyo , kikosi cha jeshi la Tanzania kikiwa na askari 450 kimesha ingia mashariki ya CONGO kwenye mji wa UVIRA SOUTH KIVU huku Kamanda wao (TPDF) akiwa mjini Goma. 



Kikosi cha jeshi la SOUTH AFRICA kiko mita 20 kutoka waasi walipo kwenye mji wa MUNGI nje kidogo ya GOMA. 


Pia aliwaeleza wananchi hao kuwa kuna makomandoo 30 wa jeshi la Ufaransa ambao wako mjini GOMA na  wamefikia Linda Hotel...


BUSIMWA alidai wafaransa ndio walisimamia mauaji ya kimbari ya Rwanda ,kwa hiyo kuwepo kwao ni ishara mbaya kwa wakazi wa mashariki ya CONGO ambao wengi ni watusi.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger