Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » MKURUGENZI WA SIMON GROUP LTD AUNGANISHWA KESI YA IDD SIMBA YA UHUJUMU WA UCHUMI

MKURUGENZI WA SIMON GROUP LTD AUNGANISHWA KESI YA IDD SIMBA YA UHUJUMU WA UCHUMI

tangazo

Mkurugenzi  Mtendaji wa Kampuni ya Simon Group Limited, iliyonunua hisa za Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam, Robert Simon Kisena ameunganishwa katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Bodi ya UDA, Idd Simba na wenzake.

Sambamba na hatua hiyo, Simba na wenzake ambao walikuwa wakikabiliwa na kesi ya awali ya matumizi mabaya ya madaraka, wamefutiwa kesi hiyo na kufunguliwa kesi upya  ambapo wameongezewa kosa jingine la uhujumu uchumi.

Kutokana na mabadiliko hayo, washitakiwa walisomewa mashitaka sita yakiwamo ya rushwa, uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka na kulisababishia shirika hilo hasara ya Sh 8.4 bilioni. Wakili wa Serikali, Oswald Tibabyekomya alidai mahakamani kuwa baada ya kuchambua ushahidi wamebaini kuwa makosa hayo yanaangukia katika Sheria ya Uhujumu Uchumi.

Mbali na Idd Simba ambaye ni mshtakiwa wa kwanza na Kisena ambaye ni mshtakiwa wa nne, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi namba 3 ya mwaka 2013, ni Salimu Mwaking’inda na Victor Alfred Milanzi. 


Mwaking’inda, ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo alikuwa Mkurugenzi wa UDA na Milanzi ambaye ni mshtakiwa wa tatu, alikuwa ni Meneja Mkuu wa UDA.

Washitakiwa hao walisomewa mashitaka hayo mapya jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Wakili wa Serikali, Awamu Mbagwa. Hata hivyo Kisena hakuwapo jana mahakamani wakati wenzake wakisomewa mashitaka.

Washtakiwa waliokuwapo mahakamani jana ni pamoja na Simba, Mwaking’inda na Milanzi ambao walikana mashitaka yote.

Wakili Tibabyekomya alidai kuwa Kisena hakuwapo mahakamani hapo jana kwa kuwa taratibu za kumfikisha mahakamani zilikuwa bado hazijakamilika.

Kwa mujibu wa hati ya mashitakam haya ndiyo mashitaka waliyosomewa jana:-

  1. Kula njama linawahusu Simba na Milanzi na Kisena. Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Septemba 2009 na Januari 2010, jijini Dar es Salaam, kwa pamoja walikula njama za kutenda kosa la vitendo vya rushwa, kinyume cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.
  2. Vitendo vya rushwa linamhusu Kisena peke yake, hata hivyo shtaka hilo halikusomwa kutokana na mshtakiwa huyo kutokuwapo mahakamani.
  3. Vitendo vya rushwa ambalo linawahusu Simba na Milanzi. Wakili Mbagwa alidai kuwa kati ya Septemba 2009 na Januari 2010, walikubali kupokea Sh320 milinoni kutoka kwa Kisena ushawishi wa kuiuzia Simon Group hisa za UDA ambazo zilikuwa bado hazijagawiwa.
  4. Matumizi mabaya ya madaraka, linawahusu Simba, Mwaking’inda na Milanzi.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger