Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » , , » "SIJAJA BONGO KUFUATA PENZI LA DIAMOND"...AVRIL

"SIJAJA BONGO KUFUATA PENZI LA DIAMOND"...AVRIL

tangazo
jana ilikuwa ni birthday ya msanii wa Ogopa Djs ya Kenya, Judith Nyambura Mwangi a.k.a Avril ambaye alitua jijini dar es salaam juzi na sababu ya ujio wake ilikuwa ni vitu vikubwa viwili.

Akihojiwa katika kipindi cha XXL kupitia Clouds fm Avril amesema ujio wake hapa bongo kwanza ni ku-celebrate birthday yake na fans wa Tanzania, na pili ni ku-launch single yake mpya aliomshirikisha Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa yuko ziarani barani Ulaya, party ilifanyika usiku wa kuamkia jana (April 30) pale Elements club.

Kuhusiana na maneno ambayo yamekuwa yakisemwa juu ya tetesi za kuwepo kwa mahusiano baina yake na Diamond Platnumz ambaye alimshirikisha Avril katika video ya Kesho, Avril amekana kuwepo kwa uhusiano wowote zaidi ya kuwa marafiki wa kawaida na wa kikazi. "Hakuna kitu chochote kati yangu na diamond  na  sijaja  Tanzania  kufuata  penzi  lake... we are just friends na relationship yetu ni proffesional relationship katika muziki", alisema Avril.
 
Hii ndo birthday party ya kwanza kwa Avril kufanya, birthdays zake zote zilizopita alikua anasheherekea kwa kuchill tu nyumbani na familia yake.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger