Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » UTAFITI: SODA NI SUMU KULIKO SIGARA....

UTAFITI: SODA NI SUMU KULIKO SIGARA....

tangazo
Mamilioni ya watanzania wanaotumia vinywaji aina ya soda ipo hatarini baada ya kugunduliwa uwepo wa chembechembe zenye kemikali za sumu ndani ya vinywaji hivyo, MTANZANIA jumatano linaripoti.

Utafiti uliofanywa na Muungano wa Waandishi wa habari Tanzania (Investigative Journalists Union of Tanzania-IJUTA) pamoja na tafiti zilizofanywa na wataalamu waliobobea katika afya duniani umebaini kuwa vinywaji baridi aina ya
soda ni hatari kuliko utumiaji sigara inayosabisha maradhi ya kansa katika mwili wa binadamu.

Kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi, yapo madhara makubwa ya utumiaji wa vinywaji vya aina ya soda katika mwili wa binadamu.


Utafiti umeonyesha kuwa zipo sababu nane kuu zinazokiweka kinywaji cha soda kwenye kundi la vinywaji vyenye sumu.


IJUTA imebaini kuwa makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji kuwa makampuni yanayotengeneza soda yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada kijamii kutokana na mauzo yake, bila kutaja madhara ya vinywaji hivyo.


Utafiti wa IJUTA umeonyesha kuwa utamu wa kupindukia uliomo ndani ya soda unawapumbaza wanywaji ili wasisikie ladha kali ya acid iliyomo ndani ya soda.


IJUTA imegundua kuwa kiwango cha acid kilichomo ndani ya soda hakiwekwi wazi kwa sababu ya kuhofia kuwa watu wakibaini wataacha kutumia kinywaji hicho.


Inaelezwa kuwa madini ya cola yaliyomo yana kilevi cha aina ya kafein kinachomteka mnywaji kuwa teja wa kinywaji hicho.


Dr. Mercola wa Marekani amekaririwa na tafiti mbalimbali akieleza kuwa
soda ni hatari kwa binadamu sawa na mtu anayevuta sigara au zaidi.

...Soda yenye chembe za cola husababisha figo kuwa na mawe kwa sababu ya acid na chemicals zinazofichwa vipimo vyake kwa watumiaji.


Wakati utafiti huo ukidhihiriksha hayo, Taasisi ya chakula na Dawa Tanzania
(TFDA) imeshindwa kutoa tamko lolote kuhusu utafiti huo, hata baada ya kupelekewa maswali kwa maandishi yanayoomba ufafanuzi wa ubora wa vinywaji vya soda katika mwili wa binadamu.

SOURCE: MTANZANIA
ISSN
: 0856-5678, Na. 7310
Toleo la leo

ukurasa wa 3

TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger