tangazo
Shehena ya samaki tani 22.5 kutoka nchini China wanaodaiwa kuharibika na kutokuwa salama kwa matumizi ya binadamu wamekutwa katika eneo la Tabata Bima jijini dar es salaam huku baadhi ya samaki hao wakiwa tayari wamekwishaingizwa sokoni kwa kuuzwa.
Baada
ya kuwepo kwa fununu za uingizwaji wa samaki waodaiwa kuharibika kutoka
nje ya nchi na kuingia hapa nchini na kuatarisha maisha ya walaji,ITV
iliendelea kufuatilia tetesi hizo kwa kushirikiana na maafisa wa mamlaka
ya chakula na dawa nchini-Tfda...
Lengo la ufuatiliaji huo lilikuwa ni kuwabaini wahusika wa samaki hao ambapo kwa eneo la tabata bima jijini dar es salaam kontena mbili zilikutwa zikitumika kuhifadhia samaki wa aina tofauti ...
Katika kontena ya kwanza inayomilikwa na kampuni ya SAIS Boutique inadaiwa iliingiza samaki aina ya vibua tani 22.5 kutoa china julai 2013 na kwa bahati mbaya samaki hao wamedaiwa kuharibika licha ya kuwa walishaanza kuuzwa sokoni tangu walipofika.

Afisa
uhusiano wa mamlaka ya chakula na dawa nchini -Tfda Bi Gaudencia
Simwanza,ameeleza kusikitishwa kwa uwepo wa samaki hao waliharibika
katika kontena hiyo huku akiongeza kuwa kontena nyingine mali ya kampuni
ya Amasa Fish Traders iliyokuwa na samaki tani 27 aina ya vibua na
kolekole kutoka nchini Yemen lazima ichunguzwe pia ili kubaini usalama
wa samaki hao.
Mmiliki
wa kontena iliyokutwa na samaki zilizoharibika Bwana Sadick
Maporo,alikiri samaki wake kuharibika lakini akadai kuwa samaki hao
waliharibika baada ya kufika hapa nchini kutokana na kukatikakatika kwa
umeme.
Mamlaka ya chakula na dawa tfda wamedai hawajatoa idhini ya samaki hao kuhifadhiwa katika kontena hizo huku barua iliyoonyeshwa na mmiliki wa kontena hiyo haikuonyesha taarifa ya Tfda kama walikagua samaki hao walipofikishwa hapa nchini jambo linalotia shaka