Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » Mpenzi wangu ni MSAGAJI, bado nampenda na kumwacha nashindwa.Naomba ushauri

Mpenzi wangu ni MSAGAJI, bado nampenda na kumwacha nashindwa.Naomba ushauri

tangazo

Dunia yetu kwa sasa imepata mabadiliko makubwa sana, kiasi cha kusababisha tamaduni na desturi zetu kuathiriwa na mabadiliko hayo.

Ingawa ni maeneo mengi yameathirika kutokana na athari za kiutandawazi, lakini kwenye hii mada ningependa kuzungumzia hawa wanawake "wasagaji ".

Binafsi ni miongoni mwa waathirika wa hayo mabadiliko ya kiutandawazi, kwa kuwa binti ambae nimempenda kwa kipindi cha hivi karibuni ndio michezo yake hiyo (usagaji), hivyo katika mahusiano yetu hapo awali, hali ilikuwa ngumu sana maana hata siku moja HAKUPENDA tuongelee mambo ya ngono ingawa ni  mpenzi wangu.

Licha ya hivyo, mara kwa mara amekuwa akizungumzia sana mabinti wenzake wakati wa mazungumzo yetu, ingawa nimekuwa nikijitahidi sana kumtoa kwenye mazungumzo hayo, ila yeye amekuwa akilazimisha tujadili mambo ya aina hiyo, hali iliyonipelekea nikawaulize hao rafiki zake kuhusu hali halisi ya mpenzi wangu. Majibu yalikuwa kama ambavyo nilitarajia (kuwa demu wangu ni msagaji).

Aidha, ikitokea nimetoka nae "out" kula nae raha kwenye maeneo ya starehe, kila aonapo rafiki zake ni lazima awatathmini kwa ukaribu mpaka watu walioko karibu yake wanatambua ni nini anafanya, mara nyingine uenda mbali zaidi mpaka kugusa wenzake maeneo ya makalio kwa kuwachapa kofi.

Sasa ndugu zangu, katika hali kama hii, nifanye nini?, maana kiukweli ni fedheha kuwa na binti anaetamani wanawake wenzake .


Mdau  JF

TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger