tangazo
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akionesha bunduki iliyokamatwa mbele ya waandishi wa habari(hawako pichani)inayodaiwa kutumika katika mauaji ya bilionea wa madini Erasto Msuya.

Bunduki inayodaiwa kutumika katika mauaji hayo.

Pikipiki mbili zinazodaiwa kutumika katika mauaji ya bilionea wa madini Erasto Msuya.
*******************
JESHI
la polisi mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kunasa bunduki aina ya SMG
yenye namba za usajili KJ10520 inayoaminika kutumika katika mauaji ya
mfanyabiashara bilonea wa madini ya Tanzanaiti , Erasto Msuya (43)
aliyeuawa kwa kupigwa risasi 13 kifuani Augosti 7 mwaka huu Mijohoroni
wilayani Hai.
Mbali
na bunduki hiyo jeshi hilo pia limefanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa
wengine wanne wanaodaiwa kuwa ni watuhumiwa muhimu katika mipango ya
mauaji ya mfanyabiashara huyo anaye aminika kuwa na vitega uchumi vya
kutosha katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana ofisini kwake,kamanda wa polisi mkoa wa
Kilimanjaro,Robert Boaz,aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni ,Sadick Mohamed
Jabir(32) mkazi wa jijini Dar es salaam na Lang’ata
wilaya ya Hai na Karim Issa Kihundwa(33) mkazi wa Lawate wilayani Siha ambao wanatajwa kuwa ni muhimu katika mauaji hayo.
Alisema
watuhumiwa hao wawili walikamatwa eneo la Kaliua wilaya ya Sikonge
mkoani Tabora wakiwa kwa mganga wa kieneyeji wakifanyiwa zindiko ili
wasitiwe mbaroni na baada ya kuhojiwa na polisi walieleza jinsi
walivyoshiriki mauaji hayo na mahali walipoficha silaha na pikipiki
zilizotumika katika tukio hilo.
Boaz
aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Jalila Zuberi Said(28) mkazi wa
Babati mkoani Manyara pia anaishi wilaya ya kondoa mkoani Dodoma na
Joseph Damas Mwakipesile maarufu kwa jina la ‘Chusa’(35) ambaye pia ni
mfanayabiashara wa madini ya Tanzanite anayeishi Jijini Arusha ambaye
anashikiliwa na jeshi hilo kwa zaidi ya wiki mbili sasa.
Alisema
jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata pikipiki nyingine inayodaiwa
kutumika katika tukio hilo yenye namba za usajili T751 CKB aina ya
KINGLION rangi nyeusi ambayo wakati wa tukio ilikuwa ikitumia namba za
bandia.
Kamanda
Boaz alisema Bunduki iliyokamatwa ilikutwa ikiwa imefichwa kwneye
tindiga katika eneo la Boroi kwenye mpaka wa wilaya za Hai na Siha huku
akiendelea kutoa wito kwa wananchi wapenda amani
mkoani Kilimanjaro,kuendelea kutoa ushirkiano kwa jeshi hilo katika
kukomesha uharifu.

