tangazo
Maneno haya yametoka kwenye ukurasa wa facebook wa mbunge Zitto Kabwe na yamesemwa na viongozi wa Chadema kama Dr Wilbroad Slaa,Edwin Mtei na Mabere Marando kuhusu waraka uliosambaa kumhusu Zitto Kabwe.
Hii ni Post ya Zitto Kabwe aliyoiweka facebook
Dr. Willbrod Slaa : ” Hatuna tatizo hata kidogo na Zitto Kabwe. Huyu
ni Naibu Katibu Mkuu wetu kama kuna tatizo jambo ambalo ameleta
tutamaliza kwa mujibu wa taratibu na tutaendelea na kazi na umoja wetu”
” Waraka huo mchafu umeandikwa na viongozi wa CCM na kutoka idara
nyeti ya serikali. Chama kitapata taarifa zao na kuanika majina yao na
nafasi zao”
Edwin Mtei : ” Haya mambo hayatubabaishi tunajua ni uongo uliotungwa
ili kutugombanisha. Kesho unaweza kusikia Zitto amehongwa hiki au kile.
Keshokutwa ukasikia Slaa amehongwa hiki baadaye Mbowe amefanya hivi
lengo kutuvuruga”
Mabere Marando: ”Andishi hili ni feki nimeliangalia andishi lote.
Nimejiridhisha kwamba limetengenezwa na watu wasiotakia mema Chadema”
Msimamo wa Zitto Kabwe:
Maneno mazuri sana yenye ukweli mtupu. Hata hivyo hekaya hii
imesambazwa na wanachama wa CHADEMA na mmoja ni kiongozi wa mkoa na
akaweka kwenye blogu yake. Viongozi wengine waka ‘like’ kwenye jamii
forums. Hawa wametumwa na usalama na CCM?



