tangazo
Mwili wa Marehemu Dk. Sengondo Mvungi ukifanyiwa maombi mara
baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
leo.
Wanachama wa NCCR-Mageuzi wakiwa wamelibeba sanduku
lililohifandhi mwili wa kiongozi huyo wa NCCR-Mageuzi na Mjumbe wa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba Mpya.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akiwa uwanjani hapo.
Mjane wa Marehemu, Bi Anna Mvungi akiwa uwanjani hapo kuupokea mwili wa mumewe
MWILI wa marehemu Dkt. Sengondo Mvungi umewasili nchini Tanzania hivi punde kutoka nchini Afrika Kusini alipofia akiuguza majeraha baada ya kuvamiwa na kukatwa mapanga.
Dkt. Mvungi alifariki Jumanne, Novemba 12, 2013 katika Hospitali ya
Millpark jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini alikopelekwa kwa
ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa
Muhimbili (MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake
Kibamba, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi
vibaya kichwani usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013.
Ifuatayo ni ratiba ya tukio zima la kuuaga mwili wake.











