tangazo
Taarifa ya kituo cha TV cha KTN Kenya inasema washukiwa wawili wa
Ugaidi kwenye mtaa wa Eastleigh wakidaiwa kuwa miongoni mwa genge
lililoshambulia msikiti kwenye mtaa huo December 2012 na kumjeruhi
Mbunge wa Kamkunji Yusuf Hassan, wameuwawa asubuhi ya November 13 2013.
Mtaa huo ambao unaaminika kuwa chimbuko la Wanamgambo wa kundi la
kigaidi la Al Shabaab ambapo mwaka huo wa 2012 washukiwa hao
walifanikiwa kutoroka, mmoja kwa gari na mwingine kwa miguu umeshuhudia
washukiwa hao wakiuwawa na Polisi waliokua wakiwasaka kwa muda kabla ya
kuwapata.
Walioshuhudia
kisa hiki kipya wanasema Polisi walitaka wajisalimishe lakini wakagoma
hivyo wakaamua kuwaua kwa risasi kwenye mtaa huu huu wenye Wakimbizi
laki sita kutoka Somalia ambao hawajasajiliwa huku hiyo ikisemekana kuwa
njia rahisi kwa Wanamgambo wa Al Shabaab kuingia Kenya.