tangazo
Muimbaji na mtangazaji wa kipindi cha taarab cha Passion FM ‘Ambaa na Mwambao’, Nyawana ‘Matashtiti’ Fundikira amefariki dunia jana.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mume wake, Nyawana amefariki kwa
ugonjwa wa Malaria na mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake
Mwananyamala, Dar es Salaam.
Pamoja na utangazaji, Nyawana alikuwa muimbaji wa taarab pia na
alijiunga na Tanzania Moto Modern Taarab, maarufu kama T-Moto pamoja na
KINGS MODERN TAARABU.
Aliwahi pia kuwa mtangazaji wa Voice of Tabora na
nyimbo alizorekodi ni pamoja na ‘Nipo Kamili’ na ‘Umesharoga Wangapi’.
Nyawana aliyewahi kuwa Miss Tabora mwaka 1996, ameacha mume na watoto
wawili. Alizaliwa mwaka 1977 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na
kupata elimu yake msingi kwenye shule ya Zanaki huku sekondari akisoma
Masjid Quba na Al Haramain.
Baada ya hapo alisomea Uhazili kabla ya kumaliza na kusomea masomo ya
Uandishi wa Habari na Utangazaji, ambapo pia alishiriki shindano la
urembo na kunyakua taji la Miss Tabora, mwaka 1996.
Source: Bongo5