Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » Mwasisi wa CHADEMA ndugu Edwin Mtei adai kuwa chanzo cha migogoro ya chama hicho ni CCM

Mwasisi wa CHADEMA ndugu Edwin Mtei adai kuwa chanzo cha migogoro ya chama hicho ni CCM

tangazo

Mwasisi wa Chadema,Edwin Mtei amesema kuna baadhi ya watu nchini wanakesha usiku na mchana kuhakikisha wanafanya njama za kukidhoofisha na hata kukipoteza kabisa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
 
Mtei,alitoa kauli hiyo wakati chama hicho kikiwa katika wakati mgumu baada ya baadhi ya viongozi wake kushambuliana kupitia mitandao ya kijamii, huku aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Arusha,Samson Mwigamba akisimamishwa kwa madai ya kukiuka kanuni za chama hicho.
 
Akihojiwa na Mwananchi, Mtei alisema kuna baadhi ya watu kutoka Chama Tawala cha CCM wanahakikisha wanatengeneza mifarakano kila kukicha ili kukivuruga Chadema.
 
Alisema mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa kauli kuwa huenda CCM ikang”oka mwaka 2015, baadhi ya makada na viongozi wameanza kukesha wakifanya mbinu ya kukivuruga ili Chadema kisishike dola.
 
“Kuna watu wa CCM wanakesha usiku na mchana kuhakikisha wanatuvuruga, ili tusishike dola mimi nasema hawatuwezi”alisema Mtei
 
Hatahivyo,alisema kitendo cha kusimamishwa na hata kufukuzwa baadhi ya makada wa Chadema kimetokana na usaliti ndani ya chama hicho huku wengine wakikubali kutumiwa na CCM.

-Mwananchi
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger