tangazo
Marehemu Nyawana Fundikira enzi za uhai wake.
Vilio vimetawala ulipo msiba wa Nyawana Fundikira, maeneo ya Gongoni, Tabora mjini wakati waombolezaji walipokuwa wakiusubiri mwili wa aliyekuwa mwimbaji na mtangazaji wa kipindi cha taarab ‘Ambaa na Mwambao’ kinachorushwa na Passion Fm, Nyawana Fundikira ulioanza kusafirishwa jana toka jijini Dar es Salaam kuja Tabora kwa maziko..
Nyawana alifariki juzi baada ya kusumbuliwa kwa muda mfupi na malaria na upungufu wa damu ambapo ameacha mjane na watoto wawili.
Video ya baadhi waomboleza waliofika msibani.
-Video kwa hisani ya Aloyson