Muigizaji wa kike aliyeanza kuigiza filamu za kitanzania (Bongo Movies) akiwa na umri mdogo na kukulia kwenye tasnia hiyo, Elizabeth Michael aka Lulu amewakumbusha fans wake yeye na Marehemu Kanumba enzi zao walipokuwa wanafanya kazi pamoja.
Lulu amepost Instagram picha iliyochukuliwa kwenye filamu aliyoigiza
na marehemu Steven Kanumba, iliyopata umaarufu sana ‘Family Tears’.
“TBT-Family Tears”, Lulu ameandika kwenye post hiyo.
Shabiki wake anaetumia jina la julianatz kwenye instagram aliandika
kumtia moyo, kutokana na mengi yanayozungumzwa mtaani kuhusu yeye na
Kanumba na kunyooshewa vidole.
“I have always had empathy for you @hotlulumichael always remember
when people point one finger at you. Three fingers are left pointing
back at them selfs keep on taking care of your mother and brother and
close your ears to the negativity."
tangazo