Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » :WANAO DAI KUWA LULU MICHAEL KAFANYIWA SHEREHE YA KUTOKA GEREZANI NI WAONGO NA WANAMPANGO WA KUMKWAMISHA KISHERIA..:...FAMILIA YA LULU YANENA

:WANAO DAI KUWA LULU MICHAEL KAFANYIWA SHEREHE YA KUTOKA GEREZANI NI WAONGO NA WANAMPANGO WA KUMKWAMISHA KISHERIA..:...FAMILIA YA LULU YANENA

tangazo

Kulipuka kwa habari kuwa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefanyiwa sherehe na kigogo baada ya kutoka Segerea, Dar kwa dhamana, familia yake imecharuka na kudai kuwa hakukuwa na jambo kama hilo wala haifikirii kufanya hivyo

Habari za uhakika zilidai kuwa Lulu ambaye anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba, mara baada ya kuachiwa kwa dhamana Januari 26, mwaka huu, kuliibuka minong’ono kutoka kwa marafiki zake mbalimbali walioelezwa kuwa walitaka kumfanyia pati lakini ndugu walikataa.


Ilielezwa kuwa licha ya ndugu hao kukataa kumfanyia sherehe ndugu yao (Lulu), bado kuna kikundi cha watu kiliendelea kueneza taarifa za kizushi kwamba lazima kuwe na sherehe ya kumpongeza baada ya kutoka gerezani.



Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana ndani ya familia ya Lulu zilieleza kuwa taarifa zilizosambaa mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba alifanyiwa bonge la pati na kikundi hicho kama madai ya awali yalivyokuwa, hazikuwa na ukweli wowote na mbaya zaidi zililenga kumjengea Lulu mazingira magumu ya kisheria.


Akizungumza na mwandishi wetu kwa sharti la kutochorwa jina , dada wa Lulu alisema kuwa familia ilikerwa kupita maelezo na kuwepo kwa taarifa hizo huku akisisitiza kwamba hazina ukweli wowote.


“Sisi kama familia hatujamfanyia wala hatufikirii kumfanyia sherehe ya aina yoyote kwa ajili ya kumpongeza. Tunaomba ieleweke hivyo na hao wanaoeneza habari za uongo waache haraka, hatuzipendi,” alisema dada huyo.


Risasi
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger