Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » Gari moja la Msafara wa Rais Kikwete lapata ajali mkoani Geita...Waandishi wa habari wanusurika

Gari moja la Msafara wa Rais Kikwete lapata ajali mkoani Geita...Waandishi wa habari wanusurika

tangazo

Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Ziwa na waandishi watatu wa habari, wamenusurika kufa baada ya gari walilokuwa wakitumia katika msafara Rais Jakaya Kikwete, mkoani Geita kupinduka.
 
Ajali hiyo ilitokea jana asubuhi katika eneo la Nyankumbu katika Kata ya Kalangalala na ilihusisha gari aina ya Toyota Land Cruiser.
 
Ajali hiyo ilitokea muda mfupi kabla ya msafara wa Rais Kikwete kuanza safari kuelekea wilayani Nyang’wale.
 
Walionusurika katika ajali hiyo ni mwandishi Peter Fabian wa Gazeti la Rai, Frederick Katulanda wa Mwananchi, Peter Makunga wa Radio Free Afrika na Meneja wa MSD Kanda ya Ziwa, Byekwaso Tabura pamoja na dereva wa gari hilo Yungi Mkwati.
 
Akizungumza baada ya tukio hilo, Tabura alisema chanzo cha ajali hiyo ni utelezi katika eneo la lami iliyokuwa umewekwa juu ya tuta la barabara ya moramu inayoendelea kujengwa.
 
Alisema hali hiyo ilisababisha gari kupoteza mwelekeo na kupinduka.
 
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Geita, Dk Adam Sijaona, alieleza kuwa watu hao walichunguzwa na kuruhusiwa kuendelea na shughuli zao.
 
 
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger