Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


DENTI WA KIKE APEWA KICHAPO CHA MBWA MWITU BAADA YA WAZAZI WAKE KUMNASA AKIWA GEST HOUSE NA MPENZI WAKE

Mwanafunzi mmoja amefumaniwa katika nyumba moja ya wageni (guest house) hapo jana, tarehe 29/6/2013 majira ya saa nane mchana katika eneo la Yombo Vituka jijini Dar es salaam.

Hata hivyo mfumaniwa mwenzake  ( mwanaume ) hajakamatwa kwani aliponyoka na kukimbia.

Wazazi wenye  uchungu na hasira wakiwa na binti yao mara baada ya fumanizi.
Wazazi wakimpiga binti yao kwa uchungu na hasira mara baada ya fumanizi.
(Picha zote na maelezo yameletwa na Dei Misana- Wavuti.com)
TUPE MAONI YAKO

KATIBU WA CHADEMA WILAYA YA MAKETE ATUPWA JELA MIEZI 9 KWA KOSA LA KUTOTII AMRI YA POLISI


Mahakama ya mwanzo Makete mjini wilayani Makete mkoani Njombe imemuhukumu katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya hiyo Bw Godfrey Mahenge (63) kwenda jela miezi 9 kwa kosa la kutotii amri halali ya jeshi la polisi Makete

Akitoa hukumu hiyo hakimu wa mahakama ya mwanzo Makete mjini Mh. John Mpitanjia amesema mtuhumiwa huyo alitumia lugha ya matusi kwa askari polisi na kuwaita kuwa ni wauaji na kudai kuwa wametumwa na chama cha mapinduzi (CCM)


Amesema baada ya mahakama yake kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashataka, mshtakiwa alitakiwa kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani lakini kutokana na kutenda kosa hilo kwa mara ya kwanza mahakama imeamua kumfunga miezi 9 gerezani ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo..



Mshtakiwa huyo hakuwa na lolote la kijitetea na hakimu kumpatia adhabu hiyo na kusema kuwa rufaa kwa mshtakiwa ipo wazi endapo anahisi ameonewa.
TUPE MAONI YAKO

OFISI YA CCM WILAYA YA MBINGA YACHOMWA MOTO



  Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga Anastasia Amasi akionyesha sehemu iliyoanzia moto kuwaka na kukamata  pazia.

  Kama unavyoona katika picha hapo ni ndani ya ofisi baada ya moto kuwaka

Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga Anastasia Amasi anayeonekana katika picha akitoa  maelezo kwa nje ambapo walimwaga mafuta aina ya petroli dilishani na kuwasha moto
 Huu ni mlango uliomwagiwa mafuta katika upenyo kisha kuwashamoto ambao haukuleta madhara kama ilivyo kusudiwa na wachomaji.



WATU wasiojulikana wamechoma moto jengo la ofisi ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma..
 

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga Anastasia Amasi amesema kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Juni 21 mwaka huu ambapo watu wasiojulikana walichoma moto moja ya jengo la ofisi za chama hicho wilayani humo  .

Moto huo ulielekelezwa katika chumba cha ofisi ya katibu ambapo walivunja vioo na kuchoma moto mapazia lakini kabla hawajachoma vitu vilivyokuwemo ndani walikimbia na kuacha dumu lililokutwa likiwa na mafuta aina ya petroli.
 

Alisema kuwa mpaka sasa hakuna hisia zozote zinazohusiana na tukio hilo ingawa uongozi wa chama cha mapinduzi wilayani humo umeshatoa taarifa kwenye vyombo ya ulinzi na usalama ambavyo vinaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
 

Katika hatua nyingine , hali ya sintofahamu imejitokeza katika uchaguzi wa viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga baada ya halmashauri hiyo kugawanywa na kuzaliwa kwa halmashauri mpya ya wilaya Nyasa kwa kuibuka kwa vitendo vya hujuma vinavyodaiwa kufanywa dhidi ya  mgombea mmoja wa nafasi ya mwenyekiti jina lake kuenguliwa katika mazingira ya kutatanisha na kuzua maswali mengi miongoni mwa madiwani wa halmashauri pamoja na wananchi na kutaka uchaguzi huo usifanyike mpaka majina yote matatu ya wagombea yawepo.
 

Mmoja wa wananchi wa halmashauri hiyo ya wilaya ya Mbinga ambaye pia ni katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi  wa kata ya Mbinga mjini Monika John alisema kuwa hizo ni dalili za kuwepo kwa njama za wazi za kupanga safu ya uongozi ambao siyo chaguo la walio wengi bali ni chaguo la baadhi ya viongozi wa halmashauri hiyo kwa masilahi yao.
 

Akizungumzia hali hiyo katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mbinga alisema kuwa uteuzi wa wagombea wa nafasi hizo hufanywa kwa kuzingatia kanuni za chama na wenye jukumu la mwisho  la uteuzi ni uongozi wa chama ngazi ya mkoa  na yeye si msemaji wa maamuzi ya ngazi mkoa ingawa amepokea tarifa ya kusitishwa kwa uchaguzi huo mpaka taarifa nyingine itakapotolewa na ofisi ya chama ngazi ya mkoa.
TUPE MAONI YAKO

LOWASSA AMTAKA OBAMA ASIZUNGUMZIE MAMBO YA USHOGA NA NDOA ZA JINSIA MOJA AKIWA TANZANIA


Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo yaNje na Ushirikiano wa Kimataifa, Edward Lowassa, amemtahadhalisha kujiepusha na kauli za kuunga mkono ushoga.
 

Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, ameliambia NIPASHE Jumapili ofisini kwake jijini hapa jana kuwa ushoga na hai za ndoa kwa watu wa jinsia moja vinaweza `kuiharibu’ ziara yake hapa nchini.

Mapema wiki hii, Rais Obama alikaririwa akizungumzia masuala hayo yanayotajwa kuwa ni moja ya haki za msingi za binadamu, alipokuwa Senegal, lakini akapingwa.
 

“Watanzania hawatalikubali na wataendelea kushikilia uhuru na heshima walizojengewa tangu awali, kwamba ushoga na ndoa za jinsia moja havikubaliki,” alisema.

Akiwa Senegal, Rais Obama alitaka serikali za Afrika kutoa haki kwa mashoga kama inavyotoa kwa raia wengine.
 

"Ninachotegemea, I pray and hope (ninasali na kutegemea) kwamba kuhusu mashoga na ndoa za jinsia moja, Rais Obama hatarudia kauli aliyoitoa kule Senegal,” alisema.

Aliongeza, "ninasema hivi kwa sababu Tanzania hatuamini katika ushoga, na endapo utawalazimisha Watanzania, watakukatalia na kushikilia uhuru na heshima waliyojengewa toka awali."

AHIMIZA MAPOKEZI MAZURI
Hata hivyo, Lowassa aliwataka Watanzania kuiheshimu na kuitumiavema fursa ya kutembelewa na Rais Obama, hivyo wajitokeze kumlaki kwa wingi.
 

"Tutambue mataifa makubwa yanakimbilia maslahi ya karne inayofuata, kwa mfano Rais wa China, Xi Jiping siku moja baada ya kuapishwa kwake alikuja hapa nchini, " alisema.
 

Hivyo, alitoa wito kwa Watanzania kuhakikisha maslahi na fursa za kiuchumi zinakuwa za kwanza kulindwa, kwa kuwa ziara hiyo itafungua milango zaidi kwa wawekezaji kuja nchini.
 

Pia, Lowassa alisema ziara ya Rais Obama ni kielelezo cha amani na usalama uliopo, na kwamba itasaidia kuwavutia watalii na wadau wa sekta nyingine za maendeleo kuitembelea Tanzania.

KITUO CHA KIJESHI
Kuhusu hofu na tetesi kuwa ziara hiyo imelenga taifa hilo kuja hapa nchini kufungua kituo cha kujiimarisha kiulinzi, Lowassa alisema Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa tayari nchi hiyo ina kituo cha kijeshi nchini Kenya.


"Tuangalie maslahi yetu tuachane na mitazamo hasi, kama ni kituo cha kijeshi tayari kipo Kenya, tujiulize kwa nini marais wa Marekani Bill Clinton na George Bush walivyofanyaziara zao hapa nchini hawakwenda Kenya," alisema.

WALINZI WA NDANI KUWEKWA KANDO
Kuhusu ziara hiyo kutumia ulinzi wa kimataifa huku majeshi ya Tanzania yakiwekwa kando kwa ushiriki wa moja kwa moja, Lowassa alisema Rais wa Marekani ana kiwango cha juu cha ulinzi unaosimamiwa na nchiyake pekee.
 

"Ni sahihi walinzi wetu kukaa pembeni, huyu ni kama Rais wa dunia, lakini hata majeshi yetu yanafanya kazi ya ulinzi lakini sio kwamba yatakaa nyuma tu," alisema.
 

SUMAYE: TUMKARIBISHE
Naye, Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, alisema ziara ya Rais Obama haina ujumbe zaidi ya kuhimiza watu wajitokeze kumpokea.
 

Hata hivyo, Sumaye alikwepa kuzungumzia kwa undani hatua ya kuwafukuza wafanyabiashara kutoka kandoni mwa barabara, ili kupisha mapokezi ya Rais Obama.
 

“Ninachokielewa ni kuwa barabara ambazo wanapita viongozi kama Rais Obama zinatakiwa kuwa katikahali ya usalama na hivyo kutakiwa kuboreshwa,” alisema.

LIPUMBA: MAFANIKIO NI MADOGO KIUCHUMI
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, alisema mafanikio ya ziaraya Rais Obama yapo katika kujitangaza kimataifa kuliko kiuchumi.
 

Profesa Lipumba ambaye ni mchumi aliyebobea, alisema changamoto iliyopo ni kwamba bado biashara kati ya nchi mbili hizo siyo kubwa kama ilivyo kwa nchi kama China na Tanzania.
 

Alitolea mfano, mwaka 2012 bidhaa za hapa nchini zilizouzwa Marekani zilikuwa na thamani ya Dola milioni 66 ikilinganishwa na zile zilizouzwa China ambapo zilikuwa ni zaidi ya Dola milioni 500.
 

Alisema bidhaa zilizoagizwa kutoka Marekani zilikuwa na thamani ya Dola milioni 230 huku za kutoka China zikiwa na thamani ya zaidi ya Dola milioni 1,100.

"Utakubaliana nami kuwa mahusiano yetu na China ni makubwa kuliko Marekani licha ya nchi hii kutoa fursa kwetu ambazo hatujazitumia ipasavyo," alisema
 

Profesa Lipumba alisema Marekani kupitia mpango wake wa kusaidia Maendeleo ya Afrika (AGOA), ulitoa fursa kwa bidhaa za Afrika kuuzwa nchini humo bila ushuru, lakini Tanzania haikuitumia.

Pia alisema utawala wa George Bush, uliisaidia Tanzania kupitia Mfuko wa Changamoto za Milenia (Millenium Challenge Compact (MCC) kupewa Dola milioni 700 kwa ajili ya kusaidia miundombinu na ujenzi wa nyaya za umeme kutoka bandarini hadi Zanzibar.

"Pana uwezekano wa mpango wa pili wa MCC, Tanzania ikapata msaada wa kuimarisha miundombinu ya umeme, lakini pia kampuni za Marekani kuja kuwekeza hapa kwetu," alisema.
 

Alisema uwekezaji wa kampuni hizoutategemeana na wafanyabiashara wa hapa nchini pamoja na serikali kutumia fursa mbalimbali za nchi hiyo.
 

Katika hatua nyingine, Profesa Lipumba alisema ili nchi iweze kujikwamua na umasikini itatokana na jinsi itakavyotumia sera na juhudina siyo kutegemea msaada kutoka nje.
 

HOTELI ZIMEJAA
Wingi wa wageni wakiwamo watakaofika kwa ajili ya ziara ya Rais Obama, umesababisha hoteli nyingi za jijini Dar es Salaam `kujaa’.
 

Uchunguzi wa NIPASHE Jumapili ulibaini kwamba kwa zaidi ya wiki sasa, hoteli nyingi hazikupokea wageni kutokana na kile kilichoelezwa kuwa, nyingine zililipiwa ingawa vyumba havikutumika kwa wakati.
 

POLISI: WASIO NA KAZI WASIJE MJINI
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga, amewataka wananchi ambao hawatakuwa na mambo muhimu ya kufanya katikati ya jiji, wasifike huko kupunguza msongamano wa watu na magari baada ya kuwasili kwa Rais Obama.
 

Alisema, baadhi ya barabara zitafungwa kwa muda kwa ajili ya viongozi kuzitumia, hivyo kusababisha msongamano.
 

Hekaheka zimetanda jijini Dar es Salaam, ikiwa ni zaidi ya saa 24 kabla ya kuwasili kwa Rais Barack Obama.
 

Rais Obama, atawasili nchini kesho akitokea Afrika Kusini, ambapo pamoja na mambo mengine, alizungumza katika mkutano wa ‘viongozi vijana wa Afrika’ na kujibu maswali kutoka nchi tofauti.
 

Mkutano huo ulifanyika jana jioni huko Soweto nchini Afrika Kusini, ambapo alipokewaa na kujibu maswali kutoka Kenya, Uganda, Nigeria na Afrika Kusini kwenyewe.
 

Jijini Dar es Salaam, shughuli kadhaazikiwamo za ulinzi na usalama, zinafanyika kwa kasi na umakini kuhakikisha ziara ya Rais Obama inafanyika pasipo bughudha. kujibu maswali kutoka Kenya, Uganda, Nigeria na Afrika Kusini kwenyewe.
 

Jijini Dar es Salaam, shughuli kadhaazikiwamo za ulinzi na usalama, zinafanyika kwa kasi na umakini kuhakikisha ziara ya Rais Obama inafanyika pasipo bughudha.
 

Hata hivyo, sehemu kubwa inayohusu masuala ya itifaki, ulinzi na usalama yanafanywa na taasisi za Marekani, kwa kuzishirikisha taasisi za ndani kwa kiwango kidogo.
 

“Hawa jamaa (Wamarekani) wanapoingia nchi yeyote wakiwa naRais wao, shughuli nyingi na uamuzi wanafanya wao, sisi wa ndani inakuwa kushirikishwa kwa kiasi kidogo,” kilieleza chanzo cha NIPASHE Jumapili kutoka moja ya taasisi zinahusika katika ziara hiyo.
 

Maeneo kadhaa ya jijini humo, yaliendelea kudhibitiwa kwa ulinzi mkali na doria za mara kwa mara, huku kandoni mwa baadhi ya barabara wakionekana askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ).
 

Mathalani, kandoni mwa barabara ya Morogoro, eneo la Ubungo, walionekana askari wa JWTZ maarufu kama MP.
 

Shughuli nyingine zimehusisha pia operesheni zinazofanywa na polisi kwa kusaidiana na mgambo wa jiji, kuhakikisha watu na bidhaa zilizopokandoni mwa barabara zitakazotumika kwa ziara ya Rais Obama, vinaondolewa.
 

Magari yaliyowabeba polisi wenye silaha za moto na mabomu ya machozi, yalionekana katika mitaa kadhaa jijini humu, wakihakikisha operesheni hiyo inafanyika pasipo kikwazo kutoka kwa wahusika.
 

Kila palipofanyika operesheni hiyo, baadhi ya askari walifanya doria zamu kwa zamu, kuhakikisha kuwa bidhaa na watu walioondolewa, hawarejei.
 

Hata hivyo, waathirika katika operesheni hiyo walieleza kutofurahia, huku wakihoji ni kwa nini serikali haikuwaandalia mazingira mbadala kabla ya utekelezaji wake. 
 
Walisema miongoni mwao, wamekopa mitaji kutoka kwenye taasisi za kifedha, hivyo kusimamisha biashara zao ili kupisha ujio wa Rais Obama, kutawaweka katika hali ngumu kiuchumi.
 

“Ikiwa ujio wa Rais Obama unatutesa wafanyabiashara kiasi hiki, ni vigumu kuhimili maisha yetu, kwa sababu hatujui hatma yetu baada ya yeye kuondoka,” alisema mfanyabiashara Zena Rashidi wa Kariakoo.
 

Hata hivyo, wamachinga walionekana jana katika kituo cha mabasi cha Mwenge walipofukuzwa, wakiwa wanaendelea na biashara zao.

Lakini walifanya hivyo kwa tahadhali ikiwamo kushika bidhaa chache mikononi, huku wakitumia 'janja' ya kupiga kelele za 'kumsifia' Rais Obama.
 

Walisikika miongoni mwao wakisema, 'praise to Obama' na wengine wakaitikia 'aaamen'. Walifanya hivyo zamu kwa zamu, lakini haikujulisha waliashiria nini.
 


BARABARA ZAPAMBWA
Aidha, barabara zote atakazopita Obama wakati wa ziara yake zimepambwa kwa bendera za Marekani na Tanzania; huku zikinakshiwa kwa picha yake ambayo imeandikwa 'President Barack Obama' karibu Tanzania.
 

Barabara hizo ni ile ya Nyerere kuanzia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Mwai Kibaki na Bagamoyo.

NIPASHE Jumapili imeshuhudia pichana bendera hizo zikiwa zimewekwa kwenye mabango yote yaliyo barabarani kuanzia Ikulu hadi kwenye barabara hizo huku usafi wa jiji ukionekana kuimarika zaidi.
 

Jana gazeti hili lilishuhudia karibu barabara zote, vijana wanaofanyakazi ya kuweka bendera na picha ya Obama wakifanyakazi hiyo.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
TUPE MAONI YAKO

KAMERA ZA JUMBA LA BIG BROTHER ZAMUANIKA POKELLO WA ZIMBABWE AKIWA MTUPU ....

Mshiriki  wa  Zimbabwe  ( POKELLO )  katika  shindano  la  Big Brother  Africa  amejukuta  akiumbuka tena  baada  ya  kamera  za  jumba  hilo  kumuanika  akiwa  mtupu  kama  alivyozaliwa  ndani  ya  mabafu  ya  jengo  hilo...

Hii  ni  nafasi  nyingine  ya  kipekee  kwa  wafuatiliaji  wa  shindano  hilo  ambao  hawakubahatika  kuiona  sinema  hiyo ya  bure.

Kuitazama  video  ni  sharti  uwe  mtu  mzima  na  ni  hiari  pia.

TUPE MAONI YAKO

WAPENZI WADONDOKA NA KUFA WAKATI WAKIFANYA MAPENZI DIRISHANI

Wapenzi wameanguka na kufa baada ya dirisha walipokuwa wakifanyia mapenzi kufunguka ghafla nchini China.

Wawili hao wanasemekana kudondoka kutoka kwenye dirisha la jengo moja la makazi kwenye jiji la Wuhan nchini humo pale dirisha hilo walilokuwa wameegemea kufunguka.


Mashuhuda walivieleza vyombo vya habari vya China kwamba wapenzi hao walikumbatiana wakati wakianguka kwenye njia ya waenda kwa miguu nje.

Kwa mujibu wa The Sun, chanzo kimoja cha habari kilisema: "Huku wawili hao wakiwa wameshikamana vilivyo, walianguka nje ya jengo hilo."

Picha za kuogofya zimefichuliwa kwenye tovuti za nchini humo zikionesha wapenzi hao wakiwa wamefunikwa kwa mashuka na polisi.

Damu ilitapakaa kwenye njia ya waenda kwa miguu karibu na wapelelezi wanaonekana wakichunguza eneo la tukio.


Miili ya wapenzi hao ilipigwa picha karibu na baiskeli ambayo ilikuwa imelazwa chini, lakini hakukuwa na ripoti zozote kwamba yeyote chini alikuwa amejeruhiwa katika ajali hiyo.

Ripoti zinasema kwamba madirisha hayo kwenye jengo hilo la makazi yalikuwa hayana ubora unaotakiwa.

Inafikiriwa kwamba mwanaume huyo na mwanamke wanawezekana walikuwa wakijaribu kujipooza kando ya dirisha hilo ndipo tukio hilo likatokea.

Haikufahamika ni umbali gani kutoka juu wawili hao walikuwa wakati wakianguka.
 

Wuhan ni jiji maarufu zaidi lililopo katikati ya China.
Ukiwa na historia ya miaka 3,500 ni moja kati ya miji mikongwe na iliyostaarabika katika China.


zero99
TUPE MAONI YAKO

BINTI AOZA MKONO BAADA YA KUANGUKA KATIKA BAISKELI....MADAKTARI WAMESHINDWA KUUPONYA, MAOMBEZI YAHITAJIKA


Janeth Nicholaus (25)mkazi wa Rwanzari Manispaa ya Tabora akionesha mkono wake wa kulia ukiwa tayari umeanza kuoza baada ya kupata ajali ya baiskeli maarufu daladala wakati akitokea nyumbani kwenda Soko kuu la Tabora mjini ajali ambayo ilitokea kwenye makutano ya barabara ya NBC. 

Huu ndio mkono wenyewe unavyoendelea kuharibika baada ya kupita hospitali kadhaa hapa Tabora mjini na kushindikana kupona lakini sasa aliamua kufika kwenye huduma ya Maombezi  Kanisa la AGAPE MIRACLE CENTER Mwanza road Tabora manispaa kwa Mchungaji Mbagata. 

NA KAPIPIJ
TUPE MAONI YAKO

MWANAUME AKATWA MAPANGA AKIDAIWA KUCHUKUA MKE WA MTU HUKO TABORA

 
 Ramadhani Mahanga ambaye amenusurika kuuawa baada ya kukatwakatwa mapanga na kijana mwenzake anayefahamika kwa jina la Juma  Hamisi ambaye alidai anatembea na mkewe na hivyo kuchukua uamuzi wa kutaka kumuua  katika kijiji cha Isenga manispaa ya Tabora.

Baba wa kijana  Juma Hamisi ambaye anadaiwa kumkatakata  mapanga Ramadhani Mahanga akiwa amekwenda kumjulia hali katika Hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete ambako amelazwa kwa ajili ya matibabu.

NA KAPIPIJ
TUPE MAONI YAKO

"BODA BODA NI SERA YA CCM KUSAIDIA VIJANA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO YA AJIRA "..LOWASSA


WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, amesema usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda ni sera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya kusaidia kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana.

Akizungumza katika haraambee na uzinduzi wa mfuko wa waendesha pikipiki maarufu mkoani Arusha, Lowassa alisema sera hiyo ni ya kuwakomboa vijana.

Alisema kuwa kitendo cha wafanyabishara wa Arusha kujipanga kusaidia bodaboda ni mfano kwa wafanyabishara wengine nchini.

“CCM ni chama kinachotetea wanyonge, na nyinyi ni wanyonge mnaohitaji kunyanyuliwa kimaisha, kitendo hiki cha wafanyabisharaa wa Arusha ni cha kuunga mkono sera ya CCM,” alisema.

Lowassa alisema tatizo la ajira ni bomu linalosubiri kulipuka na kwamba wasipowasaidia vijana kuondokana na tatizo hilo amani itatoweka.

“Ndiyo maana CCM katika ilani yake ya uchaguzi imeliweka hilo na pia kulisisitiza katika vikao vyake vya juu vya Mkutano Mkuu pamoja na Halmashauri Kuu,” alisema.



Wafanyabiashara maarufu jijini Arusha wakiongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Diwani wa Mererani, Mathias Manga, ndiyo waliyobuni wazo hilo la kuwaanzishia mfuko vijana wa bodaboda.

Katika harambee hiyo, sh milioni 84 zilipatikana huku Lowassa pamoja na marafiki zake wakichangia sh milioni 10 na pikipiki 10
TUPE MAONI YAKO

NIKKI LEE: MWANAMKE ALIYEFANYA MAPENZI NA WANAUME 5000 NDANI YA MIAKA 9

 
Ukishangaa ya Musa utayaona ya Firauni. Wakati wapo wanawake ambao hawapati salamu barabarani, Nikki Lee, 25 amevunja rekodi baada ya kutimiza idadi ya wanaume 5,000 aliofanya nao ngono.

Nikki ambaye aliibukia katika fani ya urembo anasema alifanya vitendo hivyo kwa muda wa miaka tisa sehemu mbalimbali alizokuwa akitembelea.

Anasema alikuwa anafanya ngono katika klabu za usiku, ndani ya ndege, mbuga za wanyama, sehemu za kupaki magari, ndani ya gari, sinema na disko.

Anasema kwamba alianza kufanya hivyo tangu alipotolewa bikira yake akiwa na umri wa miaka 16.

Anasema aliweza kufanya ngono na wanaume wawili kwa siku. "Nilikuwa nasikia raha  ya ajabu na ndiyo maana nilipenda kufanya ngono wakati wote," anasema Nikki. 



Alipokuwa na miaka 21 alifikisha idadi ya wapenzi 2,289 ambao alikuwa amewaandika katika kitabu chake chekundu.

"Hakuna mwanaume aliyepita mbele yangu asinitamani kwa waliotaka kufanya nami mapenzi nilifanya hivyo, kwa sasa nimeathirika na ngono," anasema Nikki.

TUPE MAONI YAKO

SERIKALI YASHUSHA USHURU WA PETROLI....USHURU WA SIMU WAFUTWA


MFUMO mpya wa Bunge kuanza na bajeti za kisekta na kumalizia na Bajeti ya Serikali pamoja na uundwaji wa Kamati ya Bajeti, umeonesha makali yake kiasi na kuilazimisha Serikali, kushusha kodi ya petroli na kufuta ushuru wa kutuma na kupokea fedha kwa njia ya simu.


Kabla ya Serikali kufikia uamuzi huo jana saa sita usiku, Kamati ya Bunge na wabunge walivutana na Serikali mara kadha wa kadha juu ya kodi mbalimbali, na kulazimika Kamati hiyo na Serikali kukaa si chini ya mara mbili, kujadili.
Katika vikao vyao, vikao viwili vya juzi na jana, Kamati ya Bajeti inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM), na Waziri wa Fedha, William Mgimwa, naibu wake wawili na wataalamu wake wa wizarani, walikaa kujadili tofauti zao mpaka saa sita usiku.


Mvutano wa Kwanza Mvutano wa kwanza ulianza mwanzoni mwa wiki hii, baada ya Waziri Mgimwa kuanza kujibu hoja za wabunge kuhusu Bajeti ya Serikali, ambayo ilipongezwa na kupingwa na Kamati ya Bajeti.


Hoja za wabunge na Kamati ya Bajeti, zilihusu punguzo la kodi katika mishahara, petroli, huduma za simu na magari yenye umri wa kuanzia miaka 10 na kuendelea na kodi katika huduma za utalii.


Hata hivyo, Mgimwa alipokuwa akijibu hoja za wabunge kabla ya kuwaomba wapitishe Bajeti ya Serikali, aliwataka wapitishe kwanza bajeti hiyo na hizo hoja zao zijibiwe katika Muswada wa Sheria ya Fedha, hatua ambayo wabunge waliiridhia na Bajeti ya Sh trilioni 18.2, ikapita.


Hata hivyo baada ya Bajeti kupita, Mgimwa aliwasilisha Muswada huo, ambao uliacha baadhi ya kodi ikiwemo ya magari mabovu kuzidi miaka 10, ya petroli na dizeli na ya simu.


Baada ya Mgimwa kumaliza kusoma Muswada huo, Chenge huku akiungwa mkono na wabunge wengi, alipokuwa akisoma maoni ya Kamati ya Bajeti, alisisitiza baadhi ya kodi zifutwe au kupunguzwa na kuielekeza Serikali kutafuta vyanzo vipya katika ripoti ya Kamati ya Spika ya vyanzo mbadala vya mapato ya Serikali.


Vikao vya saa sita usiku Kutokana na mvutano huo, Waziri wa Fedha na Kamati ya Bajeti walikutana Jumatano wiki hii mpaka saa sita usiku na hata walipotoka, walikuwa hawajaafikiana, kiasi cha Mgimwa kuja na marekebisho kidogo, ikiwemo kuondoa kodi ya utalii, lakini Chenge akaja na msimamo katika kodi ya petroli na utumaji na upokeaji fedha kwa njia ya simu.

Baada ya maoni ya Chenge, wabunge saba walileta majedwali ya mabadiliko, na kusababisha Spika wa Bunge, Anne Makinda, kuitaka Kamati ya Bajeti, Waziri wa Fedha na hao wabunge kurudi kutafuta suluhu juzi.

Katika kikao hicho cha suluhu cha juzi Alhamisi, Kamati hiyo na Waziri, waliendelea kuvutana mpaka saa sita usiku tena ndipo wakaafikiana, ambapo jana walikuja na kauli moja.


*Suluhu
Kabla ya Mgimwa kutangaza mwafaka, Chenge alipewa nafasi na kumsifu Waziri Mgimwa kwa kuwa msikivu na mtu asiyependa makuu na kusema, wamefikia makubaliano ambayo ni habari njema kwa Watanzania.

Baada ya Chenge kutangaza habari hiyo njema, Mgimwa alisimama na kuanza na kodi ya petroli, ambapo alisema Serikali imeridhia kutoongeza ushuru wa bidhaa katika petroli wa Sh 61 na hivyo, itaendelea na ushuru uliopo wa Sh 333.

Alisema pia wameridhia kusitisha kuongeza Sh 2 katika ushuru wa bidhaa ya dizeli, na hivyo dizeli itaendelea na ushuru wa mwaka huu wa fedha unaoisha Juni 30, mwaka huu wa Sh 215.

Mafuta ya taa pia, ushuru uliokuwepo ulikuwa Sh 430 na Serikali wakati wa mvutano ilitaka uongezwe uwe Sh 475, lakini katika muafaka sasa utateremka mpaka Sh 425, na bado utasaidia kuzuia uchakachuaji wa mafuta, kwa kuwa utakuwa juu kuliko wa dizeli.

Hata hivyo, katika ushuru wa barabara unaotozwa katika petroli na dizeli, walikubaliana katika petroli uongezwe kutoka Sh 200, hadi Sh 263 na katika dizeli kutoka Sh 200 hadi Sh 263, ili barabara za vijijini zijengwe na nyingine zikarabatiwe.

Mgimwa alisema katika huduma za simu za kutuma na kupokea fedha, ushuru wa asilimia 14.5 uliokuwa uwekwe, sasa umeondolewa na utabaki katika kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi na huduma zingine za simu.

Kodi ya magari yenye umri wa zaidi ya miaka 10, kwa magari ya kawaida kutoka asilimia 20-25 na katika magari ya kazi asilimia 5, Kamati ya Bunge pamoja na kuipinga, lakini ilikubaliana na msimamo wa Serikali.

Serikali pia imekubali kuchukua ushauri wa Bunge, wa kutafuta vyanzo mbadala vya mapato kutoka katika uvuvi wa samaki katika bahari kuu, uuzaji wa mashudu nje ya nchi na katika mashirika yenye tozo za moja kwa moja kutoka katika mafuta ya petroli.

Hata hivyo, Serikali ilikataa kuondoa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, katika kuwajibika kulipa asilimia 10 ya mapato ghafi yake au ya bajeti yake ya mwaka, katika Mfuko Mkuu wa Serikali kama mashirika mengine ya umma.


*Pinda, Makinda
Baada ya kumalizika kwa mvutano huo, Muswada wa Sheria ya Fedha ulipitishwa kwa ndio na wabunge wote bila kujali vyama vyao, huku Makinda akisifu kazi ya Kamati ya Bajeti, kwamba wanastahili kupata Phd ya heshima, kwani imeibadili Bajeti ya Serikali, huku Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akisifu kuwa kazi nzuri imefanyika na kuisha salama.

“Wote mtakumbuka tumeanza Mkutano huu kwa changamoto kubwa ya mabadiliko ya mzunguko mpya wa kuwasilisha Bajeti ya Serikali na pengine kulikuwepo hoja ya mashaka kuhusu ufanisi wake. 

“Napenda kuliarifu Bunge lako tukufu kwamba tumefanya vizuri sana, wote ni mashahidi kwamba waheshimiwa wabunge wamejadili kwa kina na kutoa ushauri wao ambao kwa kiasi kikubwa umezingatiwa na Serikali,” alisema Pinda.
TUPE MAONI YAKO

SUMAYE AWAASA VIJANA KULINDA TAIFA LAO NA WASIKUBALI KUNUNULIWA MWAKA 2015


WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ametaka vijana kusimama imara kulinda na kulijenga taifa lao.


Alisitiza maendeleo ya taifa hili, katu hayataweza kusonga mbele, kama viongozi wake wataendelea kuendeleza vitendo vya rushwa na biashara ya dawa za kulevya.


Aidha, alisema ataendelea kupiga vita tatizo la rushwa lililopo nchini, licha ya suala hilo kuonekana kuwa mwiba mchungu kwa baadhi ya watu, ambao ili kujiepusha na ‘alizoziita kelele zake’. Aliwataka kujisafisha dhidi ya vitendo hivyo.


Sumaye alitoa kauli hiyo jana katika Viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam aliposhiriki mazoezi ya kujenga mwili na mamia ya vijana kutoka klabu mbalimbali za Dar es Salaam. Mazoezi hayo yaliandaliwa na Klabu ya Ukwamani iliyopo katika kitongoji cha Kawe.


Alisema vijana ndiyo hazina ya Taifa kwa ajili ya maendeleo ya baadaye. Alisema kwamba pasipokuwepo na dhamira ya dhati ya kuwajengea misingi imara ya maisha yao, ni wazi Taifa litakosa viongozi bora miaka ijayo.

Alisema ni lazima kazi ifanyike badala ya kukaa na kuwaita ‘bomu linalotaraji kulipuka’.


Alisema kumekuwa na kauli mbalimbali zinazotolewa kuhusu vijana kuwa ndiyo wanaochochea vurugu katika maeneo mengi nchini, hivyo kuwajengea taswira mbaya aliyosema kuwa si jambo la busara kwa kuwa hawajapewa nafasi katika maeneo mbalimbali ili waweze kusukuma mbele maendeleo ya Taifa hili.


“Vijana msirudi nyuma, fursa zipo nyingi endeleeni kuzitumia, pale mnapoona hakuna nafasi hiyo tumieni fursa hiyo kuwauliza viongozi walioko juu yenu, hakutakuwa na bomu linalosubiri kulipuka kama mtawekewa misingi mizuri na msikate tamaa katika hilo,” alisema Sumaye.


Kuhusu rushwa aliwataka vijana hao kuwa makini nayo kwa kuwaepuka wale wote wanaotoa fedha ili kupata uongozi na kuongeza kuwa wale watu wote wanaofanya hivyo wanakuwa na lengo lao, hivyo ni vyema wakawaepuka mapema ili kujilinda.


Alisema rushwa kwa kiasi kikubwa ndiyo inayochangia kudidimiza maendeleo ya Taifa na kwamba wanaotoa fedha wanajua ni namna gani watairudisha hapo baadaye badala ya kuwaletea maendeleo.


“Hata uchaguzi unaokuja utawaona wanajipitisha kwa kutoa fedha, khanga na vitu vingine, nawaomba mtambue kuwa anayetoa vitu hivyo jua ni wazi kuwa amejiona hatoshi katika uongozi hivyo ni vyema akaepukwa,” alisisitiza Sumaye.
TUPE MAONI YAKO

DIVA WA CLOUDS FM AMVAA TENA HUDDAH....KISA NI PENZI LA PREZZO


Kama utakua ni muumini wa twitter lazima utakuwa unajua kinachoendelea kati ya mshiriki wa BBA kutoka Kenya (2013), Huddah na mtangazaji Diva Loveness love.
kiufupi ni bif kupitia twitter kisa kikiwa ni CMB Prezzo

Katika interview iliyofanywa  na Huddah, mrembo huyo wa Kenya  amesema hana uhusiano na Prezzo, ni rafiki yake tu, na hana beef yoyote na Diva na kwanza hamfaham.

"you know mimi hupenda kutoa maoni yangu, so saa ile mi natoa maoni yangu mtu ana-judge vingine, mi sina bif na Diva, na simjui, na kama uli-notice i only replied three times."

unajua mi niliandika "lol" after seeing her tweet calling Prezzo "baby", why? i just find it funny, so yeye ndio akawa anaandika all that" amesema Huddah

kwa inavyoonekana Diva alikua akisikiliza radio wakati interview ikiendelea, na haikumchukua dakika nyingi , akaibuka  katika  mtandao wa twitter:

TUPE MAONI YAKO

OBAMA ATOA SABABU ZILIZOMFANYA ASIENDE KENYA KWA SASA... SABABU KUBWA NI KESI YA UHURU KENYATTA NA MAKAMU WAKE


US President Barack Obama said Saturday the “timing was not right” for him to travel to Kenya, his father’s homeland, during his current Africa tour, but he expected to go there many times in the future.

Obama said the new government of President Uhuru Kenyatta was still finding its feet after an election in March, and that Nairobi was “still working out issues with the international community”.

He was referring to a looming trial for Kenyatta and Vice President William Ruto at the International Criminal Court for their alleged roles in deadly violence that killed more than 1,000 people after 2007 polls.

“The timing was not right for me as president of the United States to be visiting Kenya when those issues need to be worked on,” Obama said.

But the US leader said he had visited Kenya multiple times before he was president and expected to return.

“My personal ties to the people of Kenya, by definition are going to be strong and will stay strong,” he said.

Obama’s Africa tour started in Senegal, and he is currently in South Africa. He will wrap up his week-long journey in Tanzania.

Source: Capital fm
TUPE MAONI YAKO

DOKII ATOA WIMBO WA KUMKARIBISHA OBAMA TANZANIA....


Nyimbo iliyoimbwa na Dokii yenye maadhi ya kiafrika inayo mkaribisha rais Obama. jina la wimbo OBAMA WELCOME TANZANIA
TUPE MAONI YAKO

MAOFISA WA MAREKANI WADAI KUWA WAO NDO WATAPANGA MAWAZIRI WA TANZANIA WATAKAORUHUSIWA KUSHIKANA MKONO NA OBAMA AKIJA DAR


Wakati magari 150 ya msafara wa ziara ya Rais Barack Obama yamewasili nchini, majina ya mawaziri wa Tanzania yatakayoruhusiwa kumpokea kiongozi huyo kuchujwa na makachero wa FBI.

Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Moses Malaki aliliambia gazeti hili jana kuwa matayarisho ya ujio wa Rais huyo ni kabambe na hayajawahi kutokea katika historia ya Tanzania.


Pia alisema shughuli za kumpokea Rais Obama, anayetarajiwa kutua Jumatatu saa 8:40 mchana, zitaanza asubuhi kwa maofisa wa Marekani kushika majukumu yote katika uwanja huo, ikiwemo kuongoza ndege, ukaguzi wa abiria na mizigo, kwa maana wafanyakazi wa uwanja huo kuwa likizo kwa siku mbili.


“Wamesema kuwa wao watasimamia kila kitu kuanzia wageni watakaoingia na kutoka na wataamua nani aingie na kutoka,” alisema Malaki.



Aliongeza kuwa japokuwa Mamlaka ya Anga Tanzania (TAA) inaendelea kufanya kazi zake kama kawaida, lakini Jumatatu, Wamarekani watasimamia kila kitu hadi ukaguzi wa wageni.


“Siku hiyo mwongoza ndege wa TAA, atafanya shughuli kidogo, mambo mengine yatafanywa na wao,” alisema.


Idadi ya maofisa wa Tanzania

Imebainika kuwa hata idadi ya maofisa wa Tanzania wakiwemo viongozi watakaompokea pia itapangwa na Wamarekani wenyewe.

“Wenyewe wana orodha yao na wanajua nani atakuwepo au hatakiwi kuwepo katika kundi la wageni watakaompokea Rais Obama,” alisema na kuongeza:
 

“Nilimuuliza Ofisa Usalama wa Marekani iwapo nitaweza kumwona Rais Obama, akaniambia: Utamwona ukibahatika kuwepo kwenye orodha.”
 

Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe naye alikiri kuwa mawaziri wanaotakiwa kuwepo katika msafara wa kumpokea Rais Obama ni wachache watakaochaguliwa tu na Wamarekani, baada ya kuyapitia na kuyachunguza majina hayo kwanza kabla ya kuyakubali.
 

“Hii sijawahi kuiona, hata sisi wenyewe tunateuliwa na wakishayapitia wataamua, nani aende au asiende,” alisema Chikawe.

Mwananchi
TUPE MAONI YAKO

KINACHOMFANYA MWANAUME AKOROME NA KULALA BAADA YA TENDO NI MAUMBILE NA SIYO HIARI YAKE


Jambo hili huwaacha wanawake wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali chungu mzima kama kuna mahali wamekosea au hawajawavutia wapenzi wao, pale wenzi wao wanapogeukia upande wa pili na kushikwa na usingizi punde tu baada ya kumaliza tendo la kujamiiana.

Lakini utafiti uliofanywa hivi na wanasayansi unawapa wanaume ahuweni katika kuepuka lawama hizo, kwamba, kumbe siyo hiyari yao, bali ni maumbile.

Wanasayansi hao wamebaini kwamba, kwa sababu za kimaumbile ubongo wa wanaume unawalazimisha kulala muda mfupi baada ya kushiriki tendo la kujamiiana. Katika utafiti wao wanasayansi hao walibaini kwamba, kwa jinsi ubongo wa mwanaume ulivyotengenezwa, pale wanapomaliza tendo la kujamiiana na kufika kileleni kuna eneo linalozimika na kuwafanya kupata usingizi.

Wakati hilo likitokea kwa wanawake hali ni tofauti, kwani wao hubaki wakikodolea macho dari wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali lukuki, wakijihisi kutowaridhisha wapenzi wao.

Utafiti huo ulifanyika kwa kuhusisha kipimo cha kumulika, maarufu kama scan, ambapo kilitumika kuwamulika wanaume katika ubongo wao pale wanapofanya tendo la kujamiiana na baada ya kumaliza kujamiiana na kufika kileleni na kubaini kwamba, eneo linalojulikana kama cerebral cortex, eneo linalohusika na ‘fikra’ huzimika baada ya mwanaume kufika kileleni.

"Utafiti huu unatupa matokeo ya kile kinachotokea ndani ya ubongo pale mwanaume anapofika kileleni.”
Gazeti la Mirror lilimnukuu mwanasayansi mmoja wa serikali ya Ufaransa aitwae Serge Stoleru.

“Lakini kwa wanawake inaonekana ni tofauti kabisa……” Aliongeza kusema mwanasayansi huyo.

Mwanasayansi huyo aliendelea kusema kwamba, wanawake hushangazwa sana na jambo hilo na ndio sababu hubaki wakiwashangaa wapenzi wao wanapolala baada ya kumaliza tendo il hali wao wakitaka zaidi….

Kwa hiyo hakuna sababu ya wanawake kuwalaumu tena wanaume baada ya kumaliza tendo na kulala kwa sababu hivi sasa wameshajua sababu, watuache tupumuwe…… 


Mdau..
TUPE MAONI YAKO

MIZENGO PINDA AIPIGILIA MISUMARI KAULI YAKE...ADAI KUWA SERIKALI HAITAMVUMILIA MTU YOYOTE ATAKAYEPANDIKIZA CHUKI NCHINI


Serikali imesisitiza kuwa haitavumilia kuona baadhi ya watu wanaendelea kupanda mbegu za chuki za kidini na kisiasa miongoni mwa Watanzania na imesisitiza kuchukua hatua bila huruma kuzimaliza njama hizo.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana, wakati akiahirisha Mkutano wa 11 wa Bunge hadi Agosti 27, mwaka huu.

“Nataka niwahakikishie Watanzania kuwa serikali haitavumilia hata kidogo kuendelea kupandwa mbegu za chuki na za kidini na kisiasa miongoni mwa Watanzania.


“Serikali itachukua hatua kali bila huruma kuzima njama hizi mbaya dhidi ya taifa letu…vile vile, hatua kali zitachukuliwa kwa mtu yeyote atakayebainika kuhusika bila kujali hadhi na nafasi yake katika jamii,” alisema.

Waziri Mkuu Pinda aliwasihi viongozi wa serikali, kisiasa, kidini na wananchi wote kwa ujumla, kila mmoja kwa nafasi yake kuwajibika ili kuhakikisha kuwa taifa linaendelea kuwa kisiwa cha amani na utulivu.

Aliwataka Watanzania wote kushirikiana na vyombo vya dola katika kuwabaini wahalifu hao na kukataa vitendo vya uvunjifu wa amani katika nchini.

“Kila mwenye taarifa za kuwezesha kukamatwa kwa watu wanaohatarisha amani ya nchi yetu atoe taarifa kwa Jeshi la Polisi na taarifa hizo zitafanyiwa kazi kwa umakini mkubwa na kwa maslahi ya taifa letu,” alisema.

Alisema ziko dalili ya kuwepo kwa vikundi vya watu wachache wasioitakia mema nchi ambavyo vinataka kupandikiza chuki za kisiasa na kidini miongoni mwa Watanzania na kuleta mapigano na mauaji miongoni mwao.

Alisema kwa mfano, hivi karibuni, katika kipindi cha mwaka mmoja tu uliopita pamekuwepo na matukio ya vurugu, fujo na uvunjifu wa amani katika maeneo mbalimbali ya Arusha, Mwanza, Mbeya, Mtwara, Morogoro, Singida na Iringa.
Alisema hofu ya migogoro ya kidini imetokea Zanzibar, Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Geita.

Alisema baadhi ya matukio hayo yamesababisha vifo na majeruhi ikimwemo, kujeruhiwa askari na wananchi, uharibifu wa miundombinu, uharibifu wa mazingira na mali za serikali na watu binafsi.

Alisema matukio mfululizo ya fujo, vurugu pamoja na tukio la kulipua mabomu kanisani na hivi karibuni katika mkutano wa hadhara huko viwanja vya Soweto katika Kata ya Kaloleni mkoani Arusha na katika kampeni ya Chadema katika viwanja hivyo,  yamesababisha hofu kubwa kwa wananchi na hisia ya uwepo wa tishio la kuendelea kwa vitendo vinavyoashiria ugaidi nchini.

Alisema matukio ya aina hii yakiachiwa yaendelee, uchumi wa nchi utadorora kutokana na ushiriki hafifu kwenye shughuli za maendeleo.

Kauli hiyo ya Waziri Mkuu inatanguliwa na nyingine aliyoitoa pia katika kikao cha bunge kilichomalizika ambapo alisema kwa wale wanaokadi amri halali ya Jeshi la Polisi wapigwe tu.

“Na mimi nasema wanaokaidi amri halali ya Jeshi la Polisi wapigwe tu, kwa sababu hakuna namna nyingine ya kupambana  na wakaidi zaidi ya kuwapiga”.
 

Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini(CCM), Murtaza Mangungu aliyetaka kujua ni hatua gani zinazochukuliwa na serikali kufuatia matukio ya vurugu za mara kwa mara nchini.
TUPE MAONI YAKO

VIDEO YA RAIS KIKWETE AKIONGELEA SABABU ZA OBAMA KUJA TANZANIA


Ubalozi wa Tanzania London ukishirikiana na Urban Pulse na Freddy Macha wakuletea video fupi ya Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete akizungumzia ziara ya Rais Barack Obama, alipokuwa Uingereza karibuni.
TUPE MAONI YAKO

JACK WOLPER ADAI KUWA ANAPENDA KUTEMBEA NA "SERENGETI BOYS" KWA SABABU WANAYAJUA MAPENZI UKILINGANISHA NA WATU WAZIMA WENYE PESA ZAO


Nyota wa tasnia ya filamu , Jaqueline Wolper ‘Wolper Gambe’ amedai kuwa hawapendi sana wanaume wenye fedha kwani wengi wao ni waume za watu...

Wolper anadai kuwa nao si rahisi kuonyeshwa mapenzi yao ya dhati  kwani mapenzi yao ni ya  chumbani tu...


" Unajua unapokuwa na mtu mwenye fedha zake , alafu mtu mzima, ni  lazmia  ukose  penzi la kweli kwani mapenzi yenu ni chumbani tu, hamuwezi kutembea pamoja kukaa kama vile ni wapenzi ...


"Lakini ukiwa na kijana ambaye hana pesa na wewe una kazi lazima akuonyeshe jinsi mapenzi yalivyo kwa kukuweka karibu kimahaba na wewe ukafaidi penzi kutoka kwake..

“Wanaume wengi wenye  pesa zao huniona  nina dharau, lakini mimi ni binadamu nahitaji haki yangu kama mwanamke .
 
"Kuna watu wanaamini pesa zao ndio kila kitu, kiukweli kwangu siyo hivyo , ukileta mapenzi hayo lazima unione nina dharau”,anasema Wolper Gambe.

Wolper  anadai kuwa  kuna watu ambao huwanyooshea vidole wasanii maarufu kama yeye kwa kuwaona kama vile ni Malaya lakini wanasahau kama nao ni binadamu na wanaroho kama wanadamu wengine....
 
Jack Wolper anasema wao si malaika , wanapenda na kupendwa, kwa hiyo ukimuona ana kijana Serengeti boy ujue ni kwa ajili ya kupata penzi nzito na kusikilizwa haja zake.
TUPE MAONI YAKO

HUYU NDO MSANII WA BONGO MOVIE ANAYEDAI KUWA YEYE NI BIKRA NA HAMJUI MWANAUME


Mwigizaji wa kike anayetesa katika tasnia ya filamu Bongo Diana Rose kimaro ‘Diana’ amedai kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yoyote na wala hafikirii kuwa na Boyfriend kwani yeye bado ni mwanafunzi na akili yake yote ipo katika masomo .


Wakati ukifika akiwa na maisha yake atachagua ni mwanaume yupi anastahili kuwa naye kwa maisha yake rasmi lakini si sasa.
 
“Sijui kabisa mambo hayo na sijawahi kufanya upuuzi huo, ninaheshimu sana familia yangu baba yangu ni mkali sana hataki ujinga. Kwa hiyo si rahisi kudili na wanaume, mimi ni  bikira , natoa nafasi kwa masomo kwanza sitaki kujichanganya na kuwa kituko mjini,” anasema Diana.
TUPE MAONI YAKO

NAY WA MITEGO AMPARAMIA PANCHO NA KUDAI NI SHOGA BAADA YA KUTOBOA JICHO LAKE MITHILI YA BINTI MREMBO ANAYESAKA BWANA

Kuna  beef  la  chini chini  kati  ya  Pancho  na Nay wa Mitego baada  ya  Nay  kudai  kuwa  Pancho ni SHOGA...!!

Madai  ya  ushoga  yameibuka  baada  Linah  kuweka  picha  akiwa  na  Pancho  studio.Katika picha  hiyo, Pancho  anaonekana  katoboa  JICHO  mithili  ya  BINTI  MREMBO  anayesaka  mwanaume  wa  kumwondolea  "mawazo"....

Baadhi  ya  mashabiki  wamemuunga  mkono  Nay  na kudai  kuwa  huo  ndo  mwanzo  wa  ushoga kwa  watoto  wa  kiume.


Baadhi  yao  wamempinga  nay  na  kudai  kuwa  hayo  ni  maamuzi  ya  mtu.Kama  vipi  nayeye  "atoboe  makalio  yake"



TUPE MAONI YAKO

DPP ASHINDWA KUMSHITAKI SUGU KUTOKANA NA MAPUNGUFU YA HATI YA MASHITAKA..... SUGU YUPO HURU


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Dodoma Mjini, jana ilimuachia huru Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (41), maarufu kama Sugu aliyefikishwa mahakamani kwa kosa la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya hati ya mashtaka kuonesha mapungufu.

Kutokana na uamuzi huo wa Mahakama imeutaka upande wa mashtaka kurekebisha hati hiyo na kumfikisha tena mshtakiwa mahakamani huku Wakili wa Mbilinyi, Tundu Lissu akitaka kesi mpya itakayoletwa mahakamani iwe na maelezo ya Waziri Mkuu na awe tayari kusimama mahakamani kuthibitisha shitaka hilo.

Kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Elinaza Luvanda.

Awali akimsomea mashtaka, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Harriet Lopa alidai kuwa Juni 24, mwaka huu, Mbilinyi akiwa Dodoma alituma ujumbe wenye lugha ya matusi kwa kutumia mtandao wa kijamii wa Facebook kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.


Mshtakiwa alikana shitaka hilo. Hata hivyo wakili wa Mshtakiwa, Lissu aliomba kutoa hoja na kusema hati ya mashtaka ni mbovu na kuomba Mahakama itupilie mbali kwa sababu ina makosa.

“Lugha ya matusi haikutajwa, lugha gani hiyo ya matusi na hati ya mashtaka iko kimya, mshtakiwa atajitetea vipi,ataandaa utetezi namna gani kwani hata kinachodaiwa kuwekwa kwenye facebook hakijasemwa,” alidai Lissu.


Akijibu hoja hiyo, Wakili wa Serikali alisema kesi hiyo bado iko kwenye upelelezi na kutaka mshtakiwa aendelee na mashtaka yake mpaka itakapothibitishwa vinginevyo.


Kutokana na kauli hiyo ya wakili wa Serikali, Lissu alizidi kusisitiza hati ya mashtaka haina maelezo ya kutosha na inatakiwa kukidhi matakwa ya sheria.

“Hati ya mashtaka iliyoletwa si halali kinyume na kifungu cha 132 cha mwenendo wa makosa ya jinai na itakuwa makosa kama Mahakama ikikubali hati hiyo,” alisema.


Alitoa uamuzi wa Mahakama, Hakimu Luvanda alisema anakubaliana na maelezo ya Wakili upande wa utetezi Lissu kuwa hati hiyo ina mapungufu.

Alisema Mahakama inamuachia huru mshtakiwa na upande wa mashtaka unaweza kumshtaki tena mshtakiwa kama itaona umuhimu wa kufanya hivyo.

Akizungumza nje ya Mahakama Lissu alisema hati ya mashtaka dhidi ya Mbilinyi kuwa alitoa lugha ya matusi kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda haijaeleza anachodaiwa kusema Mbilinyi.


Alisema Mahakama imetenda sawasawa kuifuta hati hiyo ilitakiwa ifafanue lugha ya matusi iliyotumika ni ipi. ”Hakimu hajasema Sugu hana makosa, lakini upande wa mashtaka ukajipange kutengeneza hati mpya,” alisema.
TUPE MAONI YAKO

MAMIA NCHINI AFRIKA KUSINI WAJITOKEZA KATIKA MAANDAMANO YA AMANI YA KUPINGA KUJA KWA RAISI OBAMA


 Waandamanaji Nchini Afrika Kusini wakiwa wamebeba mabango yanayopinga kuja Kwa Raisi Obama nchini Humo wakati wa maandamano ya Amani ya Kupinga Kuja Kwa Obama Katika Jiji la Pretoria Nchini Afrika  jana Jioni - Juni 28

 Waandamanaji Nchini Afrika Kusini Wakisali mbele ya Bango linalopinga Kuja kwa Raisi Obama Nchini Humo wakati Raisi Obama alipotua Nchini Afrika Kusini Jioni ya jana  Juni 28

 Waandamaji wa Nchini Afrika Kusini wakiwa wanasali mbele ya Ubalozi wa Marekani wakati wa maandamano ya kupinga kuja kwa Raisi Obama Nchini Humo jana  wakati Raisi Obama alipotua Nchini Humo Kwa Ziara ya Siku 2 ..

Mmoja wa waandamaji nchini Afrika Kusini ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akiwa amebeba moja ya Bango ambalo Linamwita Raisi OBAMA kuwa ni Mpishi wa Ikulu ya Marekani kama linavyosomekana na kuendelea kuelezea kuwa sera za Marekani ni tatizo.Mwandamaji huyu alibeba bango hilo jana  Juni 28 wakati wa maandamo ya amani kuelekea mbele ya Ubalozi wa Marekani NChini humo kwa kupinga Kuja Kwa OBAMA Nchini Mwao.Picha Zote na REUTERS/AFP
TUPE MAONI YAKO
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger