Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Breaking News: Mawaziri 4 wavuliwa nafasi zao usiku huu bungeni


Rais Jakaya Kikwete leo ametengua uteuzi wa mawaziri wanne kufuatia shutuma nzito dhidi yao katika sakata la Operesheni Tokomeza Ujangili. 

Mawaziri waliopoteza ajira zao usiku huu ni pamoja na Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), David Mathayo (Mifugo na Uvuvi), Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani) na Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na JKT).
 
Akizungumza Bungeni Dodoma usiku huu, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikiri kulikuwa na matatizo makubwa katika usimamizi wa zoezi hilo.
 
“Tulifanya operesheni kwa nia nzuri,” alisema Waziri Mkuu Pinda  na  kuongeza : “Tatizo ni namna operesheni hiyo ilivyotekelezwa.”
 
Katika mdahalo uliogusa nyoyo za wabunge na wachambuzi mbalimbali wa siasa leo, wabunge waliueleza umma jinsi ambavyo Operesheni hiyo ilitumika kutesa, kunyanyasa na kuua raia wasio na hatia na kuwadhulumu mali zao.
Related Posts Widget For Blogger with ThumbnailsBlogger Templates TUPE MAONI YAKO

Tume ya Katiba kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Mhe. Rais Desemba 30 2013 katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam

 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Mhe. Rais

Tume ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi na wadau wengine wote kuwa Hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Dkt. Ali Mohammed  Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi itafanyika siku ya Jumatatu, Desemba 30, 2013 katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, taasisi za kidini, asasi za kiraia na wananchi wa kawaida.

Taarifa zaidi kuhusu hafla hii zitatolewa baadaye.

Imetolewa na:

Imetolewa na:
Assaa Rashid,
Katibu,
Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
Dar es Salaam
Desemba 19, 2013.

TUPE MAONI YAKO

Waziri Magufuli na Steven Wassira waongoza maelfu ya wananchi katika mazishi ya mwenyekiti wa CCM mkoa wa mwanza aliyeuawa na wananchi


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa (CCM), Clement Mabina (56), amezikwa mchana huu shambani kwake Kanyamati, Kisesa mkoani Mwanza. 

Mazishi hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, viongozi wa serikali, madhehebu ya dini, vyama vya siasa, wananchi na wakazi wa Kisesa ambao wameungana na ndugu, jamaa na marafiki kumsindikiza marehemu Mabina.
 
 
 
 
 
TUPE MAONI YAKO

Habari njema: Rais Kikwete amesaini Hati ya Dhararua ya kufanya marekebisho kwenye muswada wa fedha ili kuondoa kodi ya laini za simu


Habari za kodi kwa laini za simu ilichukua vichwa vya habari kwa wakati wake hadi pale mheshimiwa Rais alipotoa agizo kwa wahusika kulishughulikia suala  hilo....

Naibu Waziri mwenye dhamana ya mawasiliano,sayansi na teknolojia “January Makamba” ametoa habari mpya na nzuri  kuhusu kodi hii....
 
Kupita ukurasa wake wa facebook,Makamba  ameposti  huu  ujumbe:
 “Mheshimiwa Rais ametia sahihi Hati ya Dharura (Certificate of Emergency) kufanyika marekebisho kwa Muswada wa Fedha wa mwaka 2013 kuondoa tozo ya kodi kwa laini za simu (SimCard Tax). Asante Mheshimiwa Rais.”

TUPE MAONI YAKO

Lulu akumbushia enzi zake na marehemu Kanumba


Muigizaji wa kike aliyeanza kuigiza filamu za kitanzania (Bongo Movies) akiwa na umri mdogo na kukulia kwenye tasnia hiyo, Elizabeth Michael aka Lulu amewakumbusha fans wake yeye na Marehemu Kanumba enzi zao walipokuwa wanafanya kazi pamoja.
 
Lulu amepost Instagram picha iliyochukuliwa kwenye filamu aliyoigiza na marehemu Steven Kanumba, iliyopata umaarufu sana ‘Family Tears’.
 
“TBT-Family Tears”, Lulu ameandika kwenye post hiyo.
Shabiki wake anaetumia jina la julianatz kwenye instagram aliandika kumtia moyo, kutokana na mengi yanayozungumzwa mtaani kuhusu yeye na Kanumba na kunyooshewa vidole.
“I have always had empathy for you @hotlulumichael always remember when people point one finger at you. Three fingers are left pointing back at them selfs keep on taking care of your mother and brother and close your ears to the negativity."
 
Katika hatua nyingine, Lulu amelalamika kupitia akaunti yake ya twitter:
TUPE MAONI YAKO

"Mimi si waziri mzigo "...Waziri wa Elimu afunguka


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, ameamua kuvunja ukimya na kueleza kuwa yeye si waziri mzigo na wala hashtushwi na jina hilo kwani hawezi kuzuia maamuzi ya watu kumuita hivyo.

Dk. Kawambwa amesema yeye ni mchapakazi na tayari juhudi za kiutendaji katika wizara anayoiongoza zimeanza kuonekana.

Amesema kuwa suala la kuitwa waziri mzigo linatokana na yeye kuwa kioo na dira ya wenzake  katika wizara hiyo na hivyo majina kama hayo hayawezi kukwepeka na wala kuathiri utendaji wake na kujivunia kuwa yeye ni mmoja wa wasimamizi wa upatikanaji bora wa elimu hapa nchini.

 Waziri Kawamba aliamua kuvunja ukimya huo wakati akifungua kikao cha kazi cha maofisa elimu wa mikoa na halmashauri kinachojadili maendeleo ya elimu ya msingi hapa nchini pamoja na kufanya udahili wa pamoja katika matokeo ya darasa la saba.

"Kuna mtikisiko mkubwa katika wizara yetu na mengi yanasemwa wote mnasikia na Watanzania wanafahamu. Tupo katika safari nzito lakini ili gari liondoke, lazima kwanza litikisike, hivyo msiwe na wasiwasi tutafika salama tu," alisema Dk. Kawambwa.

Alisema anashangazwa kuitwa mzigo kwani kutokana na uwajibikaji wake katika wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu, wamepata mafanikio makubwa hususani katika kuinua kiwango cha ufaulu wa wanafunzi mtihani wa taifa wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2013.

 Alisema kutokana na jitihada zake na kushirikiana na watendaji na wadau mbalimbali, kiwango cha ufaulu mwaka 2013 kwa wahitimu wa elimu hiyo ya msingi

kimeongezeka kutoka asilimia 31 mwaka uliopita hadi kufikia asilimia 50.61 mwaka 2013 ambao ufaulu huo ni ongezeko la asilimia 19.89 ukilinganishwa na mwaka jana.

Waziri Kawambwa alisema jumla ya watahiniwa 844,938 walifanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi na kati yao 427,606 sawa na asilimia 50.61, wamefaulu kwa zaidi ya alama 100 kati ya 250 matokeo ambayo aliyaita ni mazuri.

Alisema kuwa kati ya watahiniwa hao waliofaulu, wasichana ni 208,227 sawa na asilimia 46.68 na wavulana ni 219,379 sawa na asilimia 55.01kitu ambacho kimeinua kiwango cha ufaulu.

Hata hivyo, alisema ufaulu huo bado haujafikiwa lengo la mpango wa Matokeo Makubwa Sasa la kufikia asilimia 60, lakini kutokana na jitihada na kipindi kifupi tangu mpango huo utangazwe, ni wazi kuwa kazi imefanyika na kustahili kupongezwa.

SOURCE: NIPASHE
TUPE MAONI YAKO

Dr. Slaa amlipua Mwenyekiti wa Halmashauri


Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbrod Slaa, amemshukia Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, Elias Kafyenda, kutokana na tabia ya kutumia magari ya serikali kwenye shughuli zake binafsi kwa lengo la kujijenga kisiasa.

Amesema atalifikisha suala hilo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia.

Dk. Slaa alilazimika kulizungumzia suala hilo baada ya kupewa taarifa kuwa Mwenyekiti huyo anatumia magari ya serikali kubeba wanachama wa CCM kijijini kwake kuwapeleka kwenye msiba na shughuli mbalimbali za kichama.

Taarifa ambazo zilipatikana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo, Makamu Mwenyekiti huyo aliamua kuwabeba wananchi kwa magari ya halmashauri ili kuhujumu mkutano wa Chadema usiweze kufanikiwa.

“Diwani anabeba watu kwenda kwenye msiba kijiji jirani kila kunapokuwa na mkutano wa Chadema, kwanini habebi wananchi kunapotokea misiba ya walalahoi hafanyi hivyo?”alihoji.

Dk. Slaa alisema waraka wa serikali unakataza kutumika kwa magari ya serikali kwenye shughuli binafsi na kwamba CCM imekumbatia yote hayo bila kuchukua hatua kwa viongozi wanaokiuka utaratibu wa serikali.

Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Magharibi, Shaban Mambo, alisema Makamu Mwenyekiti huyo ni dhaifu ndiyo maana anakimbiza watu wasiweze kushiriki mkutano wa Chadema.

Naye Afisa wa Chadema anayeshughulikia Sera na Utafiti, Waitara Mwita, alisema diwani huyo ni mzigo ndani ya halmashauri hiyo, hivyo wananchi wasikubali kumchagua kiongozi kama huyo kwa mara nyingine.

Hata hivyo, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Kafyenda, akizungumza na NIPASHE kwa simu alipoulizwa alisema madai hayo hayana msingi.
SOURCE: NIPASHE
TUPE MAONI YAKO

CHADEMA waikataa Rufaa ya Zitto Kabwe....Wamesema kuwa wanataka waamue kwanza hatima ya Uanachama wake ndo waipitie rufaa yake


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema hakitashughulikia rufaa iliyokatwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kwa Baraza Kuu kupinga uamuzi wa Kamati Kuu (CC) wa kumvua nyadhifa zake katika chama, hadi hapo itakapopitia utetezi wake na kuamua hatima ya uanachama wake katika chama hicho.

Pia kimethibitisha kupokea utetezi dhidi ya mashitaka 11 yanayohusisha usaliti dhidi ya chama na kuwachafua viongozi wakuu kupitia waraka wa mabadiliko.

 

Mashtaka hayo yanamkabili Zitto, pamoja na aliyekuwa Mjumbe wa CC, Dk. Kitila Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.
 

Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Victor Kimesera, alisema hayo alipozungumza na NIPASHE, ofisini kwake, jijini Dar es Salaam jana.
 

Kimesera, ambaye ni Katibu Mtendaji Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chadema, alisema rufaa hiyo ni kitu kidogo, hivyo haiwezi kuanza kushughulikiwa na chama katika sakata la Zitto na watuhumiwa wenzake.
 

“Kuna (kitu) kikubwa cha mbele yake (rufaa),” alisema Kimesera akijibu swali la NIPASHE lililotaka kujua nini kinaendelea kwenye chama baada ya Zitto kukata rufaa.
 

 Kimesera alisema kitu kikubwa kuliko rufaa, ambacho kitaanza kushughulikiwa na chama ni maelezo ya utetezi wa Zitto na watuhumiwa wenzake.
 

Alisema hiyo ni kwa sababu tayari kuna hoja ya CC, ambayo inataka ijiridhishe kama Zitto na wenzake waendelee kuwa wanachama au la.
 

 Kwa mujibu wa Kimesera, baada ya Zitto na wenzake kuwasilisha utetezi wao, CC itaitishwa na kuyapitia na kisha itatoa maamuzi juu ya uanachama wao.
 
“Sasa huwezi kuongea juu ya rufaa wakati hujajua uanachama wao kwanza,” alisema Kimesera.
 
 Hivyo, alisema rufaa ya Zitto itaendelea kuhifadhiwa kwenye jalada hadi hapo hatua ya kwanza ya kupitia maelezo yao ya utetezi na kuyatolea maamuzi itakapochukuliwa. “Lazima twende kwa hatua. Kwa hiyo, hiyo (rufaa) imekaa,” alisema Kimesera.
 
 Mwanasheria wa Zitto, Albert Msando, alitaja sababu mbili za mteja wake kukata rufaa kuwa ni kukiukwa kwa taratibu za kuchukua hatua za nidhamu na sababu zilizotolewa kutokuwa sahihi.
 

Msando alitaja kifungu cha 6.5.6 cha Kanuni ya Uendeshaji ya chama hicho, akisema utaratibu uliotakiwa kufuatwa kabla ya kumchukulia hatua za kinidhamu kiongozi kwa mujibu wa Katiba na Kanuni ni kupewa kwanza mashtaka kwa maandishi ili apate nafasi ya kujibu.
 

 Alisema kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashtaka yake kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashtaka kwa maandishi.
 

Alitaja  ibara ya 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba kwamba mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili.”  
 
Alitaja vipengele vingine ni kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika na atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao ndani ya wiki mbili baada ya kusikilizwa.
 

Katika hatua nyingine, Kimesera alisema Chadema imepeleka majibu baada ya Mwigamba kupeleka barua yenye malalamiko kwa Msajili wa Vyama vya Siasa dhidi ya uongozi wa chama hicho.
 

Katika malalamiko yake, Mwigamba anadai kuwa katiba ya Chadema ilivurugwa na viongozi wa chama kwa kuondoa kinyume cha taratibu maelezo ya kifungu cha katiba ya chama yaliyokuwa yakiainisha ukomo wa vipindi viwili vya uongozi.
 

 Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, alithibitisha kupokea barua hiyo ya Mwigamba na kusema ofisi yake inaifanyia kazi.
 

 Kimesera jana aliliambia NIPASHE kuwa walipeleka majibu dhidi ya malalamiko ya Mwigamba baada ya kuagizwa na msajili kufanya hivyo kabla ya Desemba 19, mwaka huu.
 

 Katika barua yake, Mwigamba amemuomba msajili kutoa mwongozo kuhusu anachodai kuwa ni mgogoro wa kikatiba uliopo ndani ya Chadema kufuatia kipengele cha katiba kinachogusia ukomo wa uongozi kubadilishwa kinyume cha utaratibu.

 Novemba 22, mwaka huu, CC iliwavua madaraka viongozi hao na kuwataka wajieleze kwa maandishi ndani ya siku 14 baada ya kudaiwa kuhujumu chama kwa kuandika waraka wa siri unaodaiwa pamoja na mambo mengine, kuwadhalilisha viongozi wakuu wa Chadema.
 
CHANZO: NIPASHE
TUPE MAONI YAKO

Mwenyekiti wa CCM aliyeuawa na wananchi mkoani mwanza atazikwa leo


MWILI wa Mwenyekiti wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, Clement Mabina (65) unatarajiwa kuzikwa leo katika eneo la Kanyama, jirani na yalipotokea mauaji yake.  Marehemu Mabina alifariki dunia Jumapili iliyopita baada ya kutokea vurugu kubwa baina yake na wananchi wa kitongoji cha Kanyama kilichopo katika Kata la Ilemela, ambayo alikuwa Diwani wake.
 

Kabla ya kufariki marehemu Mabina alimuua mtoto Natanael Malemi (12) ambaye inadaiwa alifika katika eneo la tukio baada ya kusikia kelele za wananchi waliokuwa wakimfukuza marehemu Mabina.
 

Hata hivyo inadaiwa marehemu Mabina alimfyatulia mtoto risasi iliyompiga jichoni na kutokea kisogoni baada ya kuwaonyesha wananchi alipokuwa amejificha, lakini kwa mujibu wa mama mzazi wa marehemu Juliana Natanael (40), alisema mtoto wake alikuwa amekwenda kushuhudia tukio ndipo alipopatwa na mkasa huo.
 

Chanzo cha mauaji hayo ni eneo lililokuwa likigombaniwa na wanakijiji pamoja na Mabina ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Mwanza kati ya 2007/ 2012 kabla ya kushindwa na Dk. Anthony Diallo ambaye ndiye Mwenyekiti wa sasa.
 

Baadhi ya wananchi waliozungumza na Rai walisema eneo hilo lilikuwa na mgogoro kwa muda mrefu kutokana na Mabina kushindwa kutekeleza makubaliano na wananchi hao yakiwamo ya kuwachimbia visima kwanza kabla ya kumpa ridhaa ya kumiliki eneo hilo.
 

Mwaka jana marehemu akiwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza pia alinusurika kupigwa na wananchi hao alipofika akiwa ndani ya gari laCCM lenye namba za usajili T491 AUP, ambalo hutumiwa na Mwenyekiti wa Mkoa.
 

Vyanzo vya habari vimesema mgogoro huo umekuwapo kwa zaidi ya miaka zaidi ya mitano na ulikuwa ukiibuka na kufifia, ambapo pia kuna taarifa mgogoro huo uliwahi kufikishwa serikalini pamoja na CCM kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi, lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.
 

***Marehemu Mabina alikuwa nani?

Marehemu Clement Mabina alikuwa mfanyabiashara tangu akiwa kijana, alikuwa akifanya biashara zake baina ya Tanzania na Kenya hasa wakati ule wa uhaba wa bia nchini, ambapo alikuwa akisafirisha bia kutoka Kenya na kuziingiza nchini.
 

Baada ya kufunguliwa kwa viwanda kadhaa vya bia chini, Mabina aliamua kubadili biashara na kujikuita zaidi katika kilimo, ufugaji pamoja na kuamua kujihusisha na siasa hasa baada ya kuruhusiwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa mwanzoni mwa miaka ya 1990.
 

Marehemu Mabina kwa mara ya kwanza aligombea ubunge katika Jimbo la Magu mwaka 1995 kupitia chama cha NCCR-Mageuzi, lakini kura hazikutosha na kushindwa katika uchaguzi na mgombea wa CCM wakati huo, Ernest Nyanda.
 

Baada ya kushindwa katika uchaguzi huo mwishoni mwa miaka ya 1990, Mabina aliamua kujitoa NCCR-Mageuzi na kuhamia CCM, ambapo mwaka 2000 aligombea nafasi ya udiwani katika Kata ya Kisesa wilayani Magu na kufanikiwa kushinda kwa kishindo.
 

Baada ya kufanikiwa kushinda kiti hicho, mwaka huo pia alifanikiwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu na kisha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Serikali ya Mitaa(ALAT) Mkoa wa Mwanza.
 

Nyota yake iliendelea kung’ara katika siasa baada ya kuchaguliwa kuwa Kamanda wa Vijana wa Kata ya Magu, Mjumbe wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Mwanza (NYANZA).
 

Safari yake kisiasa iliingia dosari 2010 baada ya Kamati ya Siasa Mkoa wa Mwanza kumuwekea ngumu kuendelea na nafasi hiyo kwa kutokea vurugu baina yake na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo wakati huo, Jane Mutagurwa pamoja na baadhi ya madiwani wa Halmashauri hiyo.
 

Mwaka 2007 Mabina alifanikiwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, na kufanikiwa kuchaguliwa baada ya kuwashinda wagombea wengine wawili.
 

Alikalia kiti hicho kwa kipindi cha miaka mitano pekee, kwani mwaka 2012 alipoteza kiti hicho baada ya kushindwa na Dk. Diallo.
 
-Mtanzania
TUPE MAONI YAKO

Kituo cha polisi chachomwa moto mkoani Morogoro......Raia wawili na polisi mmoja wauawa wakati wa vurugu hizo.

Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema.( PICHA ya MAKTABA)
*****
Watu watatu, akiwamo askari polisi wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya kuzuka mapambano kati ya polisi na raia katika Kijiji cha Igwati, Tarafa ya Malinyi Wilaya ya Ulanga, Morogoro. 
 
Diwani wa Kata ya Malinyi, Said Kila aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Leon Chikwita, Andrew Likomoka na Edson Kidunda.
 
Alisema mmoja wa majeruhi Idelfonce Malenga (35), hali yake ni mbaya baada ya kupigwa risasi shavuni. Majeruhi wawili majina yao hayakufahamika mara moja.
 
Diwani Kila alisema mauaji hayo yalitokea baada ya kundi la wakulima kuvamia Kituo cha Polisi Malinyi kushinikiza kuachiwa kwa wenzao watatu waliokuwa wanashikiliwa kwa tuhuma za kumuua mfugaji mmoja wa kijiji hicho hivi karibuni.
 
“Baada ya kupata taarifa za kukamatwa kwa wenzao walifika kituo cha polisi ambako, hawakuwakuta watuhumiwa hao kwani walikuwa wamehamishiwa kituo kingine,” alisema diwani huyo.
 
Alisema katika jitihada za kulinda kituo, polisi walitoa tahadhari mbalimbali za kuwataka wananchi hao kutawanyika ikiwamo kupiga mabomu ya machozi, lakini waliendelea kukaidi amri hiyo na badala yake walizidi kujikusanya na kukivamia na kisha kukichoma moto pamoja na gari la askari lililokuwapo. Katika shambulizi hilo, ndipo mauaji hayo yalipotokea.
 
Chagonja eneo la tukio
Kutokana na tukio hilo, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema ametuma timu maalumu ikiongozwa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja kwenda kuongeza nguvu katika operesheni ya kuwasaka na kuwakamata wote waliohusika na tukio hilo.
 
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso ilisema jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa, IGP Mwema ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Morogoro hususan, Kata ya Malinyi kuwa watulivu na kuendelea kutoa ushirikiano kwa Polisi wakati uchunguzi ukiendelea.
 
Chanzo cha mgogoro
Mgogoro kati ya wafugaji na wakulima wa Igwati ulianza Desemba 13, mwaka huu wakati kundi la wananchi lilipomkamata mfugaji huyo na kumpeleka katika ofisi za kijiji.
 
Ilidaiwa kuwa baada ya kumfikisha, mtendaji wa kijiji alimfungia mtuhumiwa huyo ofisini kwake na kuanza kuhoji sababu za wananchi kumkamata jambo ambalo linaelezwa kwamba liliwakera na kuanza kumshambulia hadi kuikimbia ofisi na kumwacha mfugaji huyo ambaye alishambuliwa na kuuawa.

Kitendo cha kukamatwa na kupigwa hadi kuuawa kwa mfugaji huyo kinadaiwa kuwa kilikuwa cha kulipiza kisasi baada ya wafugaji kuvamia nyumbani kwa Mjumbe wa Kamati ya Mazingira, Victoria Marietha na kumjeruhi vibaya kisha kufariki dunia katika Hospitali ya Lugala, Malinyi alikokuwa akipatiwa matibabu. 

-Mwananchi.
TUPE MAONI YAKO

Ray C anatafuta mwanaume mwaminifu wa kumuoa.....Kama upo single na unapenda awe mkeo basi bofya hapa


STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ameibuka na kusema kuwa anahitaji mume anayemzidi umri kwa miaka kumi. 
 
Akizungumza hivi karibuni kwenye kituo kimoja maarufu cha runinga, Ray C alisema anahitaji mwanaume mtu mzima anayemzidi miaka kumi, anayejitambua na asiwe mwanamuziki kwani anaamini akiwa na mtu kama huyo uhusiano wao utakuwa mzuri kuliko ule wa awali uliokuwa wa machungu.
 
“Ninamtaka mwanaume anayenizidi miaka kumi kwani kwa sasa nina miaka 31 japokuwa kwa sasa nafanya kazi kwanza ili nirudi kwenye levo yangu na nitakuwa juu zaidi ya zamani kwa sababu najitambua japokuwa nina hamu sana ya mtoto lakini yote namwachia Mungu.
 
“Nashukuru sasa hivi niko vizuri nakumbuka  meneja wangu wa kwanza alinikataza nisiwe na uhusiano na mwanamuziki lakini ndiyo hivyo nikajikuta niko na Lord Eyes ambaye alianza kunichanganyia cha Arusha (bangi) bila mimi kujua na kujikuta ninaharibikiwa lakini nimeshamsamehe na ninamuombea heri katika maisha yake,” alisema Ray C.
 
Aidha, Ray C alisema anamshukuru Mungu kwa sababu hana mume wala mtoto kwa sababu kwa jinsi alivyokuwa mwanzo angejenga picha mbaya sana kwa mwanaye.
 
“Wakati nilipokuwa na matatizo nilijifunza mengi kwamba hakuna rafiki wa kweli kwa sababu walinipenda nikiwa mzima lakini nilipokuwa naumwa hakuna hata mmoja aliyenipigia simu kunijulia hali zaidi ya mashabiki zangu tu kwa hiyo nimebadilisha mfumo wa maisha yangu,” alisema Ray C.
 
Miezi kadhaa iliyopita, mwanamuziki huyo alitangaza kuachana na madawa ya kulevya ambayo alikiri kuwa yalimharibia mwenendo mzima wa maisha yake.
TUPE MAONI YAKO

Hausigeli anaswa AKIKOJOLEA chombo cha kumpikia chakula bosi wake....Hii ni video ya tukio hilo la huzuni


Binti  mmoja  ambaye  ni  mfanyakazi  wa  ndani ( Housegeli )  amenaswa  live  na  kamera  zilizofungwa  jikoni  na  bosi  wake  akikojoa  ndani  ya  jiko  na  kisha  kuuchukua  mkojo  na  kuuchanganya  na  chakula  cha  bosi  wake.....

Kwa  mujibu  wa  maelezo  ya  bosi  huyo (  jina  limehifadhiwa ) , kamera  hizo  za  siri  zilifungwa  jikoni  mwake  siku  chache  baada  ya  kustushwa  na  mienendo  ya  mfanyakazi  huyo.

Kuna  video  fupi  ya  hapo  chini  ya  unyama  wa  huyu  housegeli.


TUPE MAONI YAKO
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger